Imetangazwa tume ya rais ya kuchunguza jinai, rais anapambana kweli kweli kutaka kurejesha picha nzuri aliyoichafua kwa kutotaka kutoa nafasi sawa wakati wa uchaguzi. Hapa ni kama kuvaa suti mpya ya bei ghali na ukaamua kusimama jalalani.
Kama inaundwa tume ya kijinai, je tutegemee tume nyingine itakayoangalia masuala ya kijamii yaliyosababisha kadhia ya Oct 29? Tusichezee kodi za wananchi, jinai haiji kwenye haki, jinai inakuja pale masuala muhimu ya kijamii yanaposhindwa kuangaziwa na kupatiwa ufumbuzi. Utapata wapi haki ikiwa CCM wanapewa haki zaidi ya vyama vingine, utapata wapi haki ikiwa ajira ni tatizo ambalo halijapatiwa dawa sahihi, na mbaya zaidi ajira serikalini zimekuwa ni za kujuana ana upendeleo.
Utaikosaje jinai pale ambapo kwenda hospitali inaonekana ni anasa, health ineqaulities, utaikosaje jinai pale tabaka la maskini linakuwa kubwa kila kukicha na huku viongozi wakigawana minofu ya kasungura ketu bila kujali wote tunataka kula.
Viongozi wamekuwa matajiri na chanzo cha utajiri wao hakieleweki, ukihoji unaambiwa 'fanya kazi'. Kama hawajatajirika kwa kutuibia mali zetu kwanini kila siku wanaongeza mageti sehemu wanazosihi? Wanahofia nini?
Jinai haikosekani pale ambapo haki inaonekana kutoa upendeleo kwa wenye nacho na masikini wakibinywa kwa kutengenezewa sheria za kikuda za kuwambia achama ila usiongee.
Hapa Makapuku hatuongelei siasa tukiamini tunaweza kukudua kwenye umande, kumbe masika hayakuduliwi. Kudua