Hukuwahi Kuniita Kwa Jina Langu
Harakati za kukimbilia mapenzi zilinifikisha mbali sana, ndugu yenu nikatoka Mtwara hadi Dom, hapo nikakaa ila Moro ikanivutia sababu kulikuwa na muziki wa zamani unaopendwa na vijana. Ndugu yenu kijana mwenye mambo ya kizee na kwa sasa ujana unanikimbia, mvi zinakaribia kukicheka kitambi.
Mambo ya kizee yakanifanya nipende muziki wa zamani, ndugu yenu millennial ila mawazo ya kizazi cha X (mawazo machafu ukisikia X unawaza zile video zetu za kina mandingo zilizopotezwa na connection za kina Giggy Money). Kizazi X kilichotoa muziki unaoweza kuusikiliza bila kupata karaha za moyo. Na hapa ndo hoja yangu inapokuja sasa.
Mkongwe sana wa muziki wa country akienda kwa jina David Allan Coe kafariki jana, mkongwe alijua kupiga gitaa na wimbo wake " You Never Even Called Me by My Name" ullitamba sana enzi hizo, mashairi yaliyosimama sana, ukishajenga nchi kwa kunywa bia ya nne, unaenda mbele na kuanza kuimba, karaoke hiyo. Coe aliandika mashairi ya wimbo wa ukitaka sababu ya kuacha kazi "Take This Job and Shove It'
Ningepandisha fidyo hapa, lakini kama hujasoma mpaka mwisho, utawezaje kusikiliza gitaa linaloteta raha kama mshangazi aliyetoa meno ya bandia ili kupuliza inanda cha kushika na mkono.
Its almost furahiday, let it be an easy one. Tabasamu, na huna sababu ya kutoniita kwa jina langu