Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Vyombo vya Habari nchini Burundi, Gabby Bugaga amefariki dunia alfajiri ya Alhamisi Aprili 16, 2026.
Kiongozi huyo amekutwa akiwa amefariki ndani ya gari katika shamba la michikichi lililopo eneo la Kivoga, kaskazini mwa jiji la Bujumbura.
Picha zilizosambaa mitandaoni, ingawa hazijathibitishwa rasmi, zinaonyesha mtu anayedhaniwa kuwa ni Bugaga akiwa ameegemea usukani wa gari aina ya Toyota Pick Up, huku akivaa fulana ya mistari ya kijani na kaptura.
Gari hilo lilionekana kuharibiwa upande mmoja, hali iliyozua hisia kuwa huenda kulikuwa na ajali ya barabarani.
Aidha, mguu mmoja wa marehemu uliripotiwa kuwa nje ya mlango wa gari, jambo lililoongeza utata kuhusu tukio hilo.
Hata hivyo, mazingira ya kifo hicho bado hayajawekwa wazi, huku taarifa kutoka chombo cha habari cha Iwacu zikidai kuwa ufunguo wa gari hilo ulikutwa ndani ya begi badala ya kuwapo ndani ya gari, hali inayozua maswali zaidi kuhusu chanzo cha tukio hilo.
Msemaji wa Serikali ya Burundi, Jérôme Niyonzima, amethibitisha kuwa Bugaga amefariki kutokana na ajali, lakini hakutoa maelezo ya kina kuhusu ajali hiyo.
“Serikali inatoa pole kwa familia, ndugu, marafiki na wananchi wote walioguswa na msiba huu,” amesema Niyonzima, akimsifu Bugaga enzi za uhai wake kwa ujasiri na kujitolea kwake katika kulitumikia taifa hilo.