Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20260424_091928_Instagram.jpg
Screenshot_20260424_092419_Opera%20Mini.jpg
 
Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe amewaomba wananchi wa Hai kumsamehe aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya, akieleza kuwa hakuna binadamu asiye na dhambi.

Mbowe amesema hayo wakati wa ibada ya mazishi ya mama wa Mbunge wa Hai, Saashisha Mafue.
Screenshot_20260424_133508_InstaPro%20.jpg
 
"Toka nimetoka gerezani mtagundua tembea yangu imebadilika ni ya kikuu, mtagundua ongea yangu sasa ni ya heshima, mtaona kwamba Mungu ameenda kunibadilisha, nimekuwa mtu bora, yaani amekutana na mimi amenifanya kuwa chuma chake."- Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai
Screenshot_20260424_133610_InstaPro%20.jpg
 
Rais wa Kenya, William Ruto amesema nchi za Afrika Mashariki zinajadili mpango wa kujenga kiwanda cha pamoja cha kusafisha mafuta katika bandari ya Tanga, kikifanana na kile cha Aliko Dangote cha nchini Nigeria.

Ruto amebainisha kuwa kiwanda hicho kitahudumia nchi kadhaa kwa kutumia mafuta ghafi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Sudan Kusini na Uganda.

Kwa upande wake Dangote amesema yuko tayari kujenga kiwanda kama chake chenye uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 kwa siku, ikiwa serikali za nchi hizo zitatoa ushirikiano.
Screenshot_20260424_133710_InstaPro%20.jpg
 
Askari wa kikosi maalum cha Jeshi la Marekani aliyeshiriki kwenye operesheni ya kukamatwa kwa aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, amekamatwa kwa tuhuma za kuweka dau la kamari la kuondolewa kwa Maduro, kabla taarifa hiyo haijawa wazi.

Gannon Ken Van Dyke alijipatia zaidi ya TZS bilioni 1 katika kamari hiyo.
Screenshot_20260424_133756_InstaPro%20.jpg
 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amekanusha taarifa kuwa Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2027) yamehamishwa kutoka Afrika Mashariki kwenda Afrika Kusini.
Screenshot_20260424_133840_InstaPro%20.jpg
 
Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka Iran kusitisha ufadhili wake kwa kundi la Hezbollah akisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kufanikisha makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano kati ya pande husika.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Oval baada ya kusimamia duru ya pili ya mazungumzo ya ngazi ya Mabalozi kati ya Israel na Lebanon, Trump ameulizwa kama Iran inapaswa kuacha kuifadhili Hezbollah ili kufikia makubaliano hayo ambapo amesisitiza kuwa hilo ni sharti lisiloepukika.

Mazungumzo ya hivi karibuni kati ya Marekani na Iran yameendelea kujikita zaidi katika suala la Nyuklia, huku Tehran ikionekana kupinga masharti yanayolenga kuizuia kuendelea kuunga mkono makundi Washirika katika eneo la Mashariki ya Kati jambo linaloendelea kuwa kikwazo kikubwa katika juhudi za kidiplomasia.

Trump ameeleza kuwa kusitishwa kwa ufadhili wa Hezbollah na Iran ni jambo la lazima ili kufikia makubaliano ya amani na kuongeza kuwa anaamini uwezekano wa Israel na Lebanon kufikia makubaliano ya amani upo iwapo hatua madhubuti zitachukuliwa mapema mwaka huu.
Screenshot_20260424_134151_InstaPro%20.jpg
 
Mfanyabiashara Tajiri zaidi Barani Afrika, Aliko Dangote, ameonyesha dhamira ya kuwekeza na kuongoza ujenzi wa Kiwanda kikubwa cha kuchakata mafuta kwa Ukanda wa Afrika Mashariki, hatua inayotajwa kuwa inaweza kubadili mwelekeo wa Sekta ya Nishati katika eneo la Afrika Mashariki,

Dangote amesema yuko tayari kutumia uzoefu na Teknolojia ya kisasa aliyoitumia kujenga Kiwanda chake kikubwa Nchini Nigeria chenye uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 kwa siku.

Akizungumza katika mkutano wa Ufadhili wa Miundombinu uliofanyika Jijini Nairobi, Rais wa Kenya, William Ruto, amesema Nchi za Afrika Mashariki zimeanza majadiliano ya pamoja kuhusu uanzishwaji wa kiwanda hicho, ambacho kinatarajiwa kujengwa katika bandari ya Tanga Nchini Tanzania, ambapo ameeleza kuwa mradi huo una thamani ya kimkakati kwa Ukanda huo, hasa katika kuimarisha uhakika wa upatikanaji wa Nishati na kupunguza utegemezi wa nje.

Aidha, Ruto amesisitiza kuwa Kiwanda hicho kimepangwa kunufaisha Nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan Kusini na Uganda, kwa kutumia mafuta ghafi yanayozalishwa ndani ya Ukanda huo badala ya kuyasafirisha nje bila kuyachakata.

Kwa sasa, Nchi nyingi za Afrika Mashariki zimeendelea kutegemea uagizaji wa mafuta yaliyosafishwa kutoka Mashariki ya Kati, hali ambayo imeziweka katika hatari ya kuyumba kwa bei na usambazaji, hasa wakati wa migogoro ya kimataifa hususan unaoendelea huko Mashariki ya Kati, changamoto ambayo imekuwa ikiongeza gharama za maisha na kuathiri uchumi wa Nchi hizo kwa kiwango kikubwa.
.
Screenshot_20260424_134227_InstaPro%20.jpg
 
Back
Top Bottom