Wale wa miaka yangu, naam miaka ile mwalimu anaheshimika kuliko waziri, viongozi tunawaita ndugu na hospitali sindano zilikuwa zinachemshwa maharage yanasubiri.
Naam nimekumbuka miaka hiyo leo kwa sababu dunia ya wapenda muziki wa nguvu (energetic music) imempoteza Tina Turner 1939-2023. Huyu ni malkia wa muziki wa Rock and Roll.
Kacheza vibao vingi vilivyopendwa duniani na tumboni kwake ni kama alikuwa na volkano, akiimba na kucheza bila kuchosha mashabiki wake.
Napenda muziki na ndiyo maana popote panapochezwa 'bakulutu' utanikuta ninamshukuru Mungu huku mkononi nimemkamata bata asiyefugwa. Ni maisha na nimeshare na wewe muda huu sababu dunia itammiss sana Tina Turner.
Bonus. Wimbo wake maarufu aliucheza baada ya kuamua kuachana na mume wake aliyekuwa akimpiga na kumnyanyasa na tangia hapo umaarufu ulikuwa ukimuulizia kila njia utasema Nemc wanahubiri kuwa na bar zisizopiga music. Pumzika legendary TT.