Makapuku Forum

Klabu ya Wydad Casablanca imefanikiwa kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mamelodi Sundowns mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Loftus Versfeld nchini Afrika Kusini.

Wydad imetinga hatua hiyo kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya ile ya kwanza kuisha kwa sare ya bila kufungana katika Uwanja wa Mohamed V nchini Morocco.
 
Viongozi wa Serikali, wastaafu na watu mashuhuri ni miongoni mwa Watanzania walioshuhudia uzinduzi wa Ikulu mpya ya Chamwino Dodoma.

Hafla hiyo imefanyuka leo Jumamosi Mei 20, 2023 katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na Marais Wastaafu wa Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia), Jakaya Kikwete (wa kwanza kusgoto) pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.

Viongozi hao wamekutana katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Ikulu ya Chamwino iliyofanyika leo Jumamosi Mei 20, 2023 mkoani Dodoma.

 
Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Janeth Magufuli tuzo ya Rais wa awamu ya tano Hayati John Magufuli kwenye hafla ya uzinduzi wa Ikulu Chamwino iliyofanyika leo Jumamosi Mei 20, 2023 jijini Dodoma.
 
Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mama Maria Nyerere tuzo ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwenye hafla ya uzinduzi wa Ikulu Chamwino iliyofanyika leo Jumamosi Mei 20, 2023 jijini Dodoma.
Merciful Munuo.
 
Kamati ya tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya uteuzi wa wachezaji watakaowania tuzo ya beki bora wa msimu wa 2022/23 Ligi Kuu Bara.

Henock Inonga- Simba
Dickson Job-Yanga
Mohammed Hussein- Simba
Bakari Mwamnyeto- Yanga
Shomari Kapombe- Simba

 
TOP 4 KIVUMBI NA JASHO EPL
.
FT: BOURNEMOUTH 0-1 MAN UNITED
️ Casemiro
.
FT: LIVERPOOL 1-1 ASTON VILLA
️ Ramsey
️ Firmino
.
Top 4 EPL
1. Man City — 85**
2. Arsenal — 81*
3. Newcastle — 69*
4. Man United — 69*
5. Liverpool — 66
(* — viporo)

 
Kazi ngumu zilizobaki Yanga ambazo zinawasubiri Viongozi kabla ya kuanza kwa Msimu mpya ni

1. Ubingwa CAF CC
2. Ubingwa wa ASFC
3. Kumbakisha Mayele
4.Kumbakisha Nabi
5 .Wakiondoka basi kutafuta mbadala wao .

Mnasemaje hapo wadau ____?
 
Shaffih Dauda

Kwa mara nyingine tena Senegal inaendelea kutawala soka la Afrika, jana usiku Senegal imechukua ndoo ya AFCON U17 2023 baada ya kuipasua Morocco 2-1 kwenye mchezo wa Fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika nchini Algeria.

Kwa hiyo sasa Senegal ni mabingwa wa mashindano yote ya Afrika kwa timu za Taifa za wanaume! Kwa kifupi ni kwamba ndoo zote zipo kwao, AFCON, AFCON U20, CHAN, Beach Soccer na sasa AFCON U17.

2021 AFCON [senior]

2022 BSAFCON [Beach Soccer]

2023 CHAN

2023 AFCON U20

2023 AFCON U17


Ukiangalia muunganiko wa mafanikio ya soka la Senegal hauishii tu kwa timu yao ya wakubwa [senior team] ambayo inaongozwa na akina Mane, Koulibaly, Mendy lakini mafanikio yao yameshuja hadi kwa timu za vijana.

Nini kimejificha nyuma ya mafanikio ya soka la Senegal? Swali hili linaweza kuwa gumu au jepesi sana.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, Augustin Senghor [Rais wa Shirikisho la Soka Senegal] anatajwa sana kama mtu ambaye yupo nyuma ya mafanikio ya Senegal.

Pekeyake hawezi bila Serikali ya Senegal chini ya Rais wa nchi Macky Sall. Serikali ina nafasi kubwa ya kutengeneza mazingira ya mafanikio ya michezo kwa ujumla wake hususan mchezo wa soka ambapo tunaizungumzia Senegal kama taifa lililofanikiwa zaidi kwa sasa barani Afrika.

Kwenye kila mashindano ya Afrika waliyoshiriki wamebeba ubingwa, hii haitoikei kwa bahati mbaya wala kwa kubahatisha! Huwezi kubahatisha kwenye kila sehemu.

Maana yake wamejiandaa na falsafa yao inafanya kazi, ukiangalia kila timu [Senior team, U17, U20 na CHAN] zote zilikuwa na walimu wake lakini kiwango cha ushindani ni kilekile.

Kwa hiyo Senegal wanaweza kutamba kwa muda fulani kwenye soka la Afrika ikiwa nchi nyingine hazitachukua hatua kwa sababu kizazi cha Mane kikiondoka bado wana mtaji mkubwa wa vijana wa U20 na U17 ambao wanaweza kuchukua nafasi.

Sky is the limit for Senegal
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…