Farhan Jr
KWANINI CAF WANASEMA SIMBA WANAPAMBANIA NUSU FAINALI YAO YA KWANZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA NA SIO NUSU YA KWANZA YA MICHUANO AFRIKA?
Okay! Mwandishi kazi yake ni kuelimisha, kuburudisha na kuhabarisha! Vyote vitatu ni kazi ya Mwandishi, nadhini sisi tujikite kwenye KUELIMISHA kisha wengine KUBURUDISHA, its okay! Fair and Legit!
Ni hivi michuano ya klabu barani Afrika ilianza 1964 ambapo michuano mikubwa zaidi ilikuwa inatambulika kama AFRICAN CUP OF CHAMPIONS CLUBS, ambapo michuano hii ilipigwa mpaka 1997 kabla ya kuboreshwa (Rebranded).
Kwahiyo tangu 1964 mpaka hivi sasa wale wote waliotwaa ubingwa wa michuano hii wanaorodheshwa kama Mabingwa na ukienda kwenye website ya CAF mabingwa wote wapo kuanzia 1964 mpaka 2022, kwakuwa kilichobadilika ni jina na muundo tu.
SIMBA alicheza nusu fainali ya AFRICAN CUP OF CHAMPIONS CLUBS mnamo 1974 wakati huo haitambuliki kama LIGI YA MABINGWA AFRIKA lakini ipo kwenye orodha kuwa Simba walicheza nusu fainali ya michano mikubwa Afrika.
Kwanini?? Ukienda kwenye website ya CAF kupitia bando la @tigo_tanzania wanajua kuwa CAF CHAMPIONS LEAGUE awali ilitambulika kama CHAMPIONS CUP, hivyo wanawatambua tangu 1964 mpaka 2022 kama Mabingwa WINNERS OF PREMIER CAF COMPETITION, kwakuwa walibadili tu jina, hivyo wanaposema nusu fainali ya kwanza ya CAF CHAMPIONS LEAGUE ni sahihi kwakuwa Simba alicheza CLUBS CHAMPIONS CUP.
Bingwa wa Afrika 1974 ambapo Simba alicheza nusu fainali alikuwa ni CARA Brazaville ya Kongo! Hatua ya nusu fainali SIMBA VS GHAZL EL MEHALLA na CARA BRAZAVILLE VS ASC Jeanne De Arc, fainali ilawa Cara vs Mehalla.
Ukienda kwenye website ya CAF Bingwa wa 1974 ndie huyo kawekwa na nusu fainali ndizo hizo na Simba alicheza hii michuano!
Kwanini michuano ilibadilishwa? Ilikuwa muundo wa kidunia ambapo Ulaya walihama kutoka European Cup na kuita CHAMPIONS LEAGUE 1992 huku timu zikiendelea kutambulika ni Mabingwa wa Ulaya hata kama walibeba kabla ya 1992.
Issa Hayatou 1997 akabadili pia Afrika na kuita CAF Champions League huku mfumo ukibadilika kutoka knockouts mpaka hatua ya awali, makundi kisha Knockout stages! Simba alishafanya hivyo kabla ya hii format mpya.
Thats the logic! A very simple logic!