Makapuku Forum

Makapuku Forum

Magazeti ya leo April 1, 2023.
Screenshot_20230401_063031_Opera%20Mini.jpg
 
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) katika kukuza Kiswahili Kimataifa limezindua mafunzo ya stadi za kufundisha Kiswahili kwa wageni kwa Diaspora na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania - Abu Dhabi ili baadaye maofisa na diaspora hao wafundishe Kiswahili nchini humo na kwa mataifa mengine katika Falme za Kiarabu na duniani kwa ujumla na kufanya Kiswahili kizidi kukua na kuenea zaidi Duniani.

Walimu kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) akiwemo Mwalimu Arnold tayari wapo katika Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ajili ya kutoa Mafunzo ya Stadi za Kufundisha Kiswahili kwa Wageni, mafunzo hayo yatatolewa kwa Maafisa wa Ubalozi na baadhi ya Diaspora ili kupitia mafunzo hayo na wao waanze kuwafundisha Kiswahili Wageni wa Mataifa mbalimbali.

Kaimu Balozi Tanzania Abu Dhabi Hangi Mgaka na Mwenyekiti wa Diaspora Shehe Hamisi Awadhi wamezindua mafunzo ya Kiswahili kwa Diaspora na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania - Abu Dhabi kwa kukabidhi vitabu vya kufundishia kiswahili vitakavyotumika darasani.

Diaspora wamesema uwepo wa darasa hilo utawasaidia Watoto wao pia kujifunza kiswahili
Screenshot_20230401_063856_OGInsta%2B.jpg
 
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, limepokea magari mapya matatu ya kuzima moto kutoka kwa Shirika la Nyumbu lililopo Kibaha Mkoani Pwani ambalo lipo chini ya Jeshi la Wananchi na limekamilisha matengenezo ya magari hayo na yapo tayari kuanza kazi.

Magari hayo mapya yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 2.7 yenye uwezo wa kubeba maji lita 5,000/= na Foam lita 500 kwa kila gari, yamekabidhiwa kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini kutoka kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa.

Baada ya makabidhiano hayo Waziri Bashungwa @innocentbash amenukuliwa akisema “Uwekezaji wa Viwanda katika Sekta ya Ulinzi (Defence Industry) ni moja ya maono ya Mh. Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kujenga ustawi na kuimarisha Mashirika ya TATC Nyumbu na Mzinga ni kipaumbele kikubwa, nawapongeza TATC Nyumbu kwa uundaji wa magari ya zimamoto ambayo sasa yanaenda kutoa huduma kwa Wananchi kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji”

"Kuna shirika hili la Nyumbu na Mzinga yapo chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwahiyo zipo fursa za uwekezaji kwenye Wizara ya Ulinzi, walivyokuja Scania kuangalia engine wakaona utengenezaji wa bodi ya gari la zimamoto lililotengenezwa Nyumbu walishangaa sana wakaona kwa ubora huu hatuoni kwanini Tanzania iendelee kuagiza magari ya zimamoto wakati mnaweza kutengeneza hapa kwa viwango vya kimataifa na kupitiliza”

Kwa upande wake Kamishna Jenerali Masunga ametoa shukrani nyingi kwa Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kuahidi kuyatunza Magari hayo na kuendelea kuwahudumia Wananchi katika huduma za Kuzima Moto na Uokoaji.
Screenshot_20230401_063945_OGInsta%2B.jpg
 
Wizara ya Fedha na Mipango imesema kuwa Serikali imeanza mchakato wa kuandaa Dira Mpya ya Taifa ya Maendeleo (Vision 2050), ambayo itatoa maono na kuweka malengo ya Taifa kwa kipindi cha miaka 25 ijayo.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Christian Omolo, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hafla ya uzinduzi wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Aprili 3, 2023 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, jijini Dodoma.

Bi. Omolo amesea maandalizi ya Dira mpya ya 2050 yanakidhi matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuisha kwa kipindi cha utekelezaji wa Dira iliyopo sasa ya Taifa ya Maendeleo ya 2025, inayotarajiwa kumaliza muda wake baada ya miaka miwili ijayo.

“Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025 utekelezaji wake utafikia tamati mwaka 2025 ambapo hadi sasa utekelezaji wake umeliwezeshaTaifa kupiga hatua kubwa ya maendeleo katika nyanja mbalimbali hususan za kijamii, kiuchumi na kisiasa”
Screenshot_20230401_064121_OGInsta%2B.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limewataka Wananchi wa Mkoa huo kubadilisha vitasa vyao vya milango na kutotumia vinavyoning’iniza kufuli mlangoni ili kuepuka wizi katika maeneo yao kwakuwa kufuli huwafanya Wezi wajue kuwa ndani hakuna Mtu.

Akiongea na Wananchi wa Kata ya Bagara Wilayani Babati Mkoani Manyara Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara George Katabazi amesema " Hapa Bagara mnaongoza kwa matukio mengi ya kihalifu hususani kwenye uvunjaji wa nyumba za Watu pamoja na wizi, na uuzaji wa dawa za kulevya, nimebaini Wahusika ni Watoto wenu na mnaogopa kutoa taarifa kwa kuogopa lawama"

"Nimebaini kuna baadhi ya nyumba mmeweka makufuli yanayoning’inizwa mlangoni kwa nje na mnaondoka, tubadilishe utaratibu wa kuweka haya makufuli maana ni rahisi Mtu kugundua huyu Mtu hayupo, hivyo naomba tubadilishe huo utaratibu wa kuweka hizo kufuli ili mtu asigundue kwamba ndani kuna Mtu au hakuna"
Screenshot_20230401_064220_OGInsta%2B.jpg
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa taarifa kuwa Mtu binafsi au Kampuni yeyote inayotaka kuagiza vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki kuanzia tarehe 23 Mei 2023, vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki vinavyoingizwa nchini vitatakiwa kukaguliwa kwenye Nchi vinakoagizwa ili kuhakiki kuwa havijafika mwisho wa matumizi.

“Aidha, ada ya usimamizi wa taka za kielektroniki italipwa kwa kila kifaa kinachoingizwa kwa ajili ya gharama za usimamizi wa vifaa hivyo vinapofika mwisho wa matumizi kama inavyoelekezwa na Kanuni za bora wa vifaa vya Mawasiliano ya Kielekitroniki na usimamizi wa Taka za Kielekitroniki za Mwaka 2020.

“Katika kutekeleza jukumu hili TCRA imeingia kandarasi na Kampuni ya M/S BUREAU VERITASI TANZANIA LIMITED kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa vifaa vya mawasiliano ya kielekitroniki kwenye Nchi vinakoagizwa ili kuhakiki kuwa vifaa hivo havijafika misho wa matumizi pamoja na kuwezesha ukusanyaji wa ada za usimamizi wa taka za kielekitroniki, kuanzia tarehe 23 Mei 2023, maombi yote ya kuingiza vifaa vya mawasiliano ya kielekitroniki yatawasilishwa kwa nia ya mtandao kupitia https://verigates.tcra-bureauveritas.co.tz_ili kuwezesha uwasilishwaji wa taarifa zote za vifaa vinavyoagizwa”
Screenshot_20230401_064310_OGInsta%2B.jpg
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwa na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wamemuaga Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris na Mumewe Douglas Emhoff katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 31 Machi 2023 mara baada ya kuhitimisha ziara nchini Tanzania.
Screenshot_20230401_064358_OGInsta%2B.jpg
 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde amefunga mafunzo ya ufugaji jongoo bahari yaliyokuwa yakifanyika kwenye Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kampasi ya Lindi na kuratibiwa na Wizara hiyo chini ya Wakala ya Mafunzo ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kampasi ya Mkindani Mkoani Mtwara.

Mafunzo hayo ambayo yamehusisha Washiriki 68 yamefanyika kwa muda wa siku 10 ambapo kwenye hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo, Silinde amewataka kutumia ujuzi walioupata kuzalisha jongoo bahari wa kutosha ili kuongeza kipato chao na Taifa kwa ujumla.

Silinde amesema “Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa Maagizo ya Rais Samia aliyoyatoa kwenye kilele cha Maonesho ya Nanenane mwaka jana Mbeya ambapo alielekeza sekta zote za uzalishaji ikiwemo sekta ya Uvuvi kushirikisha Wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi kuwawezesha Wananchi waweze kujiajiri”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga mbali na kuishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwezesha mafunzo hayo, amewataka Wananchi wote mkoani humo kujiingiza kwa wingi kwenye uzalishaji wa mazao ya Uvuvi ikiwemo jongoo bahari ili kuendelea kuupandisha uchumi wa Mkoa kwa ujumla.

“Kilo moja ya jongoo bahari inauzwa zaidi ya shilingi 180,000 sasa kama Wananchi wote tutajikita kwenye shughuli hii bila shaka tutafika mbali sana na ninawaomba wenyeviti wa Halmashauri, Mstahiki Meya na Wakurugenzi mliopo hapa, ile 10% ya Wanawake na Vijana ni bora wapewe Wahitimi hawa wa mafunzo kwa sababu wanafanya shughuli ambayo inajulikana na faida yake inaonekana wazi”
Screenshot_20230401_064449_OGInsta%2B.jpg
 
Ofisa wa Polisi kaunti ya Kisumu nchini Kenya, ameuwa kwa kupigwa na jiwe kifuani wakati wa maandamano nchini huo yaliyofanyika jana Alhamisi Machi 30, 2023.

Ofisa huyo aliyetambulika kwa jina la Ben Oduor baada ya kupata dhoruba ya kupigwa na jiwe kifuani lililorushwa kwa manati na kupelekwa Hospitali ya Aga Khan katika chumba maalumu cha wagonjwa mahututi na baada ya muda alipoteza maisha jana usiku.

Kamanda wa Polisi eneo la Nyanza nchini humo, Noah Mwivanda amesema marehemu alirushiwa jiwe hilo kwa manati ya kutengeneza wakati polisi wakikabiliana na waandamanaji.

Screenshot_20230401_064631_OGInsta%2B.jpg
 
Kiongozi wa Jeshi nchini Uganda, Muhoozi Kainerugaba ambaye ni mtoto wa Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, amesema atatuma vikosi vya Jeshi mjini Moscow nchini Urusi kulinda usalama endapo kutatokea tishio la kiuslama nchini humo.

"Nchi za Magharibi zinapoteza muda wake kwa propaganda zisizo na maana za Kiukreni, Uganda itatuma wanajeshi kuilinda Moscow kama kutatokea uvamizi nchini Urusi," aliandika kiongozi huyo ambaye ni mfuasi wa Rais wa Urusi, Vladmir Putin kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Pia kupitia mtandao huo, kuongozi huyo mkuu wa jeshi jana alitangaza kuanzisha chaneli ya runinga yenye chapa ya jina lake ‘MK’.
Screenshot_20230401_064721_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali ya Tanzania ipo katika maandalizi ya Programu ya Uwekezaji katika Sekta ya Maji ambayo itatekelezwa kuanzia mwaka 2023 hadi 2030 na itagharimu Dola za Marekani bilioni 24.7.

Mpango huo unafuata baada ya Julai 2022 kuzinduliwa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji, Awamu ya Tatu itakayodumu miaka minne (2022-2026) ikigharimu Dola za Marekani bilioni 6.46.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema hayo katika kikao cha Bodi ya Maji ya Taifa kilichofanyika mkoani Morogoro akieleza kuwa Tanzania ina maji yanayoweza kupatikana kila mwaka wastani wa mita za ujazo bilioni 126 ambapo mita za ujazo bilioni 105 ni maji juu ya ardhi na mita bilioni 21 ni chini ya ardhi.

Mbali na kutoa taarifa hiyo, Luhemeja amewasisitiza wajumbe wa bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Katibu Mkuu mstaafu Mhandisi Mbogo Futakamba, kutumia uzoefu wao katika kutoa majibu ya changamoto zinazohusu maji na sio kuegemea katika mabadiliko ya tabianchi kwa sababu miradi ya maji inategemea uwepo wa vyanzo vya maji muda wote.

Pia, amesema kuendeleza na kutunza rasilimali za maji hapa nchini ni jambo la msingi na lenye faida kubwa kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo kama moja ya urithi katika jamii, huku akiitaka Bodi ya Maji ya Taifa kutembelea wadau na kuona changamoto zao ili kupata majibu, kufanya tathmini na kushauri ipasavyo kwa sababu huduma ya maji maana yake ni kuangalia uhai wa Watanzania.
Screenshot_20230401_064815_OGInsta%2B.jpg
 
Watu watatu wa familia moja wamefariki dunia kwa kuteketea na moto, baada ya lori lililobeba gesi kupinduka na kuwaka moto uliosambaa kwenye nyumba zao katika Kijiji cha Kwamachalima wilayani Handeni mkoani Tanga.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Henry Mwaibambe amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Machi 31, 2023 majira ya saa 11 asubuhi ambapo dereva wa lori alieleza kuwa chanzo ni kupasuka tairi ya mbele ya kushoto.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini kama ni kweli chanzo ni tayari, kwani mashaka ni mengi kutokana na tukio hilo.
Screenshot_20230401_064904_OGInsta%2B.jpg
 
Mwanamuziki wa Uholanzi mwenye makazi yake nchini Kenya, ambaye ni muuzaji mkubwa wa mbegu za kiume, pia mwenye watoto takriban watoto 550 duniani kote anakabiliwa na mashtaka ya kuongeza athari kwenye mahusiano.

Jonathan Jacob Meijer, 41, ameshtakiwa kwa madai ya kuongeza hatari ya uhusiano wa kingono kati ya ndugu wa damu.

Kwa mujibu wa gazeti la ‘New York Post’ wameeleza kuwa Meijer, anauza mbegu za kiume katika kliniki 13, zikiwemo 11 za Uholanzi, ambapo aliwekewa vikwazo mwaka 2017 kwa kuwa na watoto 102.

Kulingana na sheria za Uholanzi, wafadhili wa mbegu za kiume hawaruhusiwi kuzaa zaidi ya watoto 25 au kuwapa mimba zaidi ya wanawake 12 ili kuzuia kuzaliana, uhusiano wa ujamaa au matatizo ya kisaikolojia kwa watoto wanaogundua kuwa wana ndugu na dada wengi.

Screenshot_20230401_064954_OGInsta%2B.jpg
 
Ili kujiridhisha sababu za kifo cha Kijana Enos Misalaba (32) aliyepoteza maisha Machi 28,2023 akiwa katika kituo cha afya Mganza alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua akiwa mahabusu mwili wake umerudiwa kufanyiwa uchunguzi kabla ya kwenda kuzikwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Berthaneema Mlay amesema wamelazimika kuufanyia mwili huo uchunguzi upya ili kujiridhisha sababu zilizopelekea kifo chake na baadaye wataupeleka makaburini kwa ajili ya maziko.

Mazishi hayo yanafanywa na familia kwa kushirikiana na Serikali ya wilaya na jeshi la polisi.
Screenshot_20230401_065052_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom