Baada ya mvutano wa miezi zaidi ya miwili kuhusu masuala ya kimkataba kati ya mchezaji Feisal Salum, 'Fei Toto' na klabu ya Yanga, Jumatatu Machi 13, 2023 huenda ikawa mwisho wa sakata lote ambapo kiungo huyo anatarajia kukutana na Rais wa Yanga, Hersi Said na Mfadhili wa timu hiyo, Gharib Said Mohamed 'GSM'.
Kikao hicho kitakachofanywa kwa siri kubwa kitakuwa na ajenda mbili hadi tatu, ambapo ya kwanza ni GSM kutaka kummwagia mkwanja mrefu mchezaji huyo na kuboresha mkataba wake zaidi ya ule wa kwanza ili abaki Yanga.
Pili wataangalia namna ya mchezaji huyo anavyoweza kuvunja mkataba na kuambiwa kiasi gani cha fedha anapaswa kuwalipa Wanajangwani hao ili kuondoka kwa amani.