China imeweka rekodi mpya duniani kwa kuunda meli kubwa yenye uwezo wa kubeba makontena 24,116 pamoja na mizigo ya tani zaidi ya 240,000.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Gazeti la Umma la nchini humo leo Machi 10, 2023 kupitia mtandao wa ‘swahili people’, imeeleza kwamba kukamilika uundaji wa meli hiyo huko Shanghai, China, ni rekodi mpya ukilinganisha na meli iliyoundwa mwaka jana yenye uwezo wa kubeba makontena 24,000.
Kampuni tanzu ya Shirika la Uundaji Meli la China imesema tayari kazi ya uundaji imekamilika kwenye kituo cha uundaji wa meli cha Changxing cha Shirika la Uundaji Meli la China.
“Hii ni meli kubwa zaidi iliyoundwa na kukamilika duniani, ambayo imevunja rekodi ya “Meli ya Changyi” iliyokamilika Mwezi Juni, Mwaka 2022 yenye uwezo wa kubeba makontena 24,000,” imenukuliwa sehemu ya taarifa hiyo.