Makapuku Forum

Makapuku Forum

4d713170c50ddfb589df7025342c5f29.jpg
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohammed Janabi ameitaka Familia ya Marehemu Swalehe Mshale kufika katika Uongozi wa Hospitali hiyo ili kukamilisha taratibu za kupatiwa mwili wa Mpendwa wao.

Akiongea na @ayotv_ kwa njia ya simu Prof. Janabi amesema “Utaratibu upo very clear ni kurudi hapo kwa Watu wa social (Ustawi) kuna barua ambayo wanatakiwa kuandika ya commitment wataacha ID wataruhusiwa kuchukua mwili halafu baada ya hapo watakuwa na makubaliano kama ni miezi sita kama ni mwaka kila mtu anaji-commit kivyake kwamba atakuwa analipa kidogokidogo, hivyo wakamuone Mkurugenzi wa Uuguzi”

"Tatizo ni kwamba Watu wa namna hii hawafuati taratibu wanazotakiwa kuzifuata badala yake wanakimbilia kwenye Jamii wakitarajia tutapata pressure, we don't get pressure unajua eeeh, hizi hela ni za Serikali sasa imagine anakuja Mkaguzi CAG namwambia huyu nimemsamehe Milioni nane, huyu tisa akiniambia Janabi wewe umechukua Milioni moja hapa umeandika msamaha ushahidi upo wapi!?, ama documents ninasema huyu Mtu amesamehewa na nini...?”

Itakumbukwa mapema leo Familia ya Marehemu Swalehe Mshale (74) wa Mbagala Majimatitu, iliiomba Serikali kuwafutia deni la milioni 10 wanalodaiwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambalo limefanya wasiruhusiwe kuchukua mwili wa Mpendwa wao mochwari toka alipofariki February 10 2023.
Screenshot_20230215_181042_Instagram%20Lite.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Magharibi Unguja, Rashid Simai Msaraka amepiga marufuku Wafanyabiashara wa Wilaya hiyo kuweka midoli yenye nguo zisizo za staha nje ya maduka yao.

DC Msaraka ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na Mfanyabiashara maeneo ya Kwahani Zanzibar akiwa ameweka midoli hiyo nje ya duka ikiwa imevalishwa nguo ambazo zinadaiwa kupotosha maadili ya Zanzibar hususani kwa Watoto pindi wanapoona midoli hiyo imevishwa nguo hizo.

DC Msaraka ameiambia AyoTV kuwa maarufuku hiyo imetokana na Watoto na Vijana kuona vitu visivyo na staha na kupelekea kuvuraga akili za Vijana wa Zanzibar "Hatuwakatazi kuwa na midoli hiyo wala hatuwakatazi kufanya biashara hizo ila biashara hizo zifanywe ndani na zisiwekwe nje, Mtu anayetaka kuvaa nguo hizo avae mwenyewe anajua utaratibu gani wa kuzivaa na wapi azivae"
Screenshot_20230215_181213_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali imetoa vibali vya kuingiza mchele nchini Tani Elfu 90 kwa ruhusa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa zao hilo kwa Taifa na pia Serikali imeondoa baadhi ya kodi ili zao hilo liweze kuongezeka kwenye soko.

Waziri Kijaji ametoa kauli hiyo Dar es salaam leo ambapo amenukuliwa akisema “Tunatarajia kuanzia mwisho mwezi huu wa pili, wiki ya kwanza ya mwezi wa tatu zao la mchele litapungua bei na Watanzania waweze kufikia zao hilo na kununua katika bei inayohimilika"
Screenshot_20230215_181344_OGInsta%2B.jpg
 
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imemuachia huru Jonas Charles maarufu Mkondo Abisai Mkazi wa Wilaya ya Sikonge aliyekuwa akikabiliwa na makosa ya kuua bila kukusudia.

Akisoma uamuzi huo wa Mahakama Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora Dkt. Mwajuma Kadilu Juma amesema Mahakama imepitia hoja za pande zote mbili katika shauri hilo na kubaini kuwa Mshtakiwa alitenda kosa hilo bila kukusudia.

Amesema kwakuwa ameshakaa muda wa zaidi ya miaka sita gerezani ambao unatosha kuwa adhabu, hivyo ameachiwa huru huku akitakiwa kwenda kuishi kistaarabu na jamii pasipo kutenda makosa ya aina hiyo.

Jonas alishitakiwa kumuua bila kukusudia kwa kumchoma kisu mara tatu Willson Kaswiza mwaka 2010.

Hata hivyo upande wa mashtaka chini ya wakili Tunosye Luketa uliiambia Mahakama kuwa, Mshtakiwa alitenda kosa hilo Juni 22 mwaka 2010 baada ya kumchoma kisu zaidi ya mara tatu marehemu Willson katika vurugu zilizotokea wakati wakiwa kwenye moja ya starehe Kijiji cha Kawale, Wilayani Sikonge.
Screenshot_20230215_181744_OGInsta%2B.jpg
 
Familia ya Marehemu Swalehe Mshale (74) wa Mbagala Majimatitu A Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam, imeiomba Serikali kuwafutia deni la milioni 10 wanalodaiwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambalo limefanya wasiruhusiwe kuchukua mwili wa mpendwa wao mochwari.

Mzee Swalehe alifariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Februari 10 2023 wakati akipatiwa matibabu kutokana na utumbo wake kutoboka na hadi sasa ni siku ya tano wameshindwa kuuchukua mwili wake kwa ajili ya mazishi kutokana na deni wanalodaiwa la milioni Kumi ambapo wanasema wameambiwa watoe asilimia 75 ya deni ndipo wapewe mwili wa Mpendwa wao.

"Tulikuwa na Mgonjwa Muhimbili Hospitali alilazwa Kibasila wodi namba 11 akahamishiwa Mwaisela ICU namba 2 kwa ajili ya matibabu zaidi kwa sababu hali yake haikuwa nzuri hadi February 10 akafariki ambapo nikaambiwa nikafunge bili, nikakuta nadaiwa milioni kumi na laki sita lakini kutokana na hali yangu ngumu ya kiuchumi nikaambiwa nifate process ili tupate msamahama ambapo tuliandikiwa barua na Serikali ya Mtaa tukaenda hadi Muhimbili Ustawi wa Jamii ndipo tukaambiwa tulipe asilimia 75 ya pesa sawa na milioni nane".

"Uwezo wetu ni mdogo sana, kama Serikali inaweza kutupa mwili wetu tutashukuru sana lakini kama haiwezekani basi itabidi sisi tuache tuangalie taratibu nyingine maana hadi sasa tumefanikiwa kukusanya shilingi milioni moja tu" amesema Stumai Mshale, Ndugu wa Marehemu.

AyoTV inaendelea kuutafuta Uongozi wa Hospitali ya Muhimbili ili kusikia kutoka upande wao.
Screenshot_20230215_181851_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom