Wakati mwili wa Papa Benedict XVI ambaye alifariki dunia Jumamosi Desemba 31, 2022 katika makazi yake huko Vatican akiwa na umri wa miaka 95 imeelezwa, maneno ya mwisho aliyotamka kabla ya kufikwa na mauti ni “Bwana ninakupenda.”
Kabla ya kifo chake, kando kulikuwa na muuguzi ambaye hafahamu lugha ya Kijerumani, katibu wake, Askofu Georg Gänswein alisema. Kwamba “Benedikit XVI kwa sauti ya chini kabisa ambayo ilieleweka alisema kwa Kiitaliano ‘Signore ti amo!’ yaani “Bwana ninakupenda.”
Ofisi ya Papa ya Holy See Press, Benedict XVI ilieleza alifariki katika makazi yake monasteri ya Mater Ecclesiae ambayo aliyachagua kama makazi yake baada ya kujiuzulu mwaka 2013.
Mwili wa kiongozi huyo mstaafu duniani wa kanisa Katoliki ambaye ni raia wa Ujerumani, utazikwa Alhamisi Januari 5, 2023 kwenye makaburi yaliyoko katika kanisa la Mtakatifu Petro, Vatican ikitanguliwa na ibada ya mazishi itakayoongozwa na Papa Francis.