Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mhariri msaidizi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Ibrahim Yamola amesema tukio la kujiuzulu kwa Spika wa Bunge Job Ndugai Januari 6 ni miongoni mwa matukio yaliyoibua mjadala ndani na nje ya CCM hadi kufikia kujiuzulu.

Ndugai ambaye ni mbunge wa Kongwa aljiuzulu, baada ya kumuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akibainisha kuwa uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari ikiwa ni siku chache kupita tangu kueleza tahadhari ya serikali kuendelea kukopa nje ya nchi.
“Kabla ya Ndugai kuchukua uamuzi wa kujiuzulu wanachama na wabunge wenzake wa CCM walimshambulia na kila aina ya lugha zilitolewa. Ni tukuio la kukumbukwa.

Mara baada ya kujiuzulu, aliyekuwa naibu spika, Dk Tulia Ackson alipitishwa na CCM kuwa mgombea uspika na akashinda kuongoza Bunge” amesema Yamola

Screenshot_20221229_053234_OGInsta%2B.jpg
 
“Bajeti ya Kilimo kwa mara ya kwanza ilikuwa zaidi ya Sh900 bilioni ambayo haijawahi kutokea na imeelekezwa katika mabwawa ya umwagilijiaji.

Ruzuku kwa wakulima kutokana na upandaji wa bei ya mbolea katika soko la dunia na mbolea ambazo zimefika zimeuzwa kwa bei ya chini,

Ujenzi wa vihenge pia umeshuhudiwa, lakini kwa mara ya kwanza tumeruhusu uuzaji wa bidhaa za vyakula nje ya nchi matokeo yake tumepata mfumuko wa bei, kufungua mipaka kumefanya ushindani uwe mkubwa”- Mchambuzi wa masuala ya uchumi, Gabriel Mwang'onda

Screenshot_20221229_053323_OGInsta%2B.jpg
 
“Mwaka 2022 utakumbukwa kwa uwekezaji katika sekta ya afya ikiwemo ujenzi wa maboma zahanati na hospitali, ununuzi vifaa tiba na kusambazaa.

Pia, Mamlaka ya Dawa na Tamisemi wamekuwa wakisimamia suala la ugawaji dawa kwa ufasaha jambo ambalo limekuwa likitolewa mfano hata na Global fund wanapotaka kuzungumzia suala la usambazaji dawa”- Mchambuzi wa masuala ya uchumi, Gabriel Mwang'onda

Screenshot_20221229_053421_OGInsta%2B.jpg
 
“Mwaka 2022 tulishuhudia mambo manne, uwekezaji, kuifungua nchi, kuitangaza na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi salama kwa wawekezaji, uwekezaji katika miundombibu, Tanzania kuingia katika kundi la nchi la uchumi wa kati katika ukuaji wa chini.

Mwaka 2020 uchumi wa Tanzania ulidorola kwa sababu ya Uviko-19 na nchi nyingi ziliingia kwenye anguko la kiuchumi kwa sababu ukigusa wazalishaji wakafa na hela nyingi zikaingia katika matibabu lazima uchumi ushuke”-Mchumi Chuo Kikuu Cha Mzumbe, Profesa Aurelia Kamuzora

Screenshot_20221229_053510_OGInsta%2B.jpg
 
“Ajali ya ndege ya Precision ni jambo ambalo litaendelea kukumbukwa kwani Tanzania haijawahi kupata ajali ya ndege kubwa kiasi kile ulikuwa ni mshtuko mkubwa

Lakini hasa baada ya ajali yaliyotokea, waliibuka mashujaa wengine, kukaibika mjadala wa Majaliwa hivyo ni tukio ambalo miaka nenda tutaendelea kulikumbuka kwa sababu pia yapo mengi ambayo tunapaswa kujifunza kupitia tukio lile.

Mkutano wa siku wa vyombo vya habari duniani kwa mara ya kwanza katika historia kwa mara ya kwanza ulihudhuriaa na Rais Samia Suluhu Hassan na kushirikisha wadau mbalimbali wa habari kutoka maeneo tofauti ya dunia”-Rashid Kejo- Mhariri wa Mafunzo wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).
Screenshot_20221229_053637_OGInsta%2B.jpg
 
“Ili demokrasia ikue lazima watu waambizane, waongee watoe mawazo mbadala na chokonozi ili waliopo madarakani waelewe nini kinaendelea”-Dk Aviti Mushi wa UDSM

Screenshot_20221229_053730_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anayeendelea na matibabu nchini South Africa.

Akizungumza na Wanafamilia kwa niaba ya Rais Samia, Waziri Mkuu amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Rais na kusema anafuatilia hali ya Mstaafu Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.

Waziri Mkuu ametoa salamu hizo leo (Jumatano, Desemba 28, 2022) jijini Johannesburg, Afrika Kusini alikokwenda kumjulia hali Mstaafu huyo.

Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na Wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao ambapo Mtoto mkubwa wa Mzee Lowassa aitwae Fredrick Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.
Screenshot_20221229_053844_OGInsta%2B.jpg
 
Kuelekea mchezo wa Simba SC dhidi ya Prisons utakaochezwa Ijumaa ya December 30, 2022 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Mkurugenzi wa Silent Ocean Salaah Said Mohamed @counsellorsalaah kupitia kwa Meneja Masoko wa Silent Ocean Mohamed Kamilagwa ameahidi kuwa ataipa Prisons kiasi cha Tsh. Milioni 30 kama itaifunga Simba SC katika mchezo huo na sare ataipa Tsh. Milioni 10.

“Hawa Vijana wakipewa hamasa wana athari kubwa sana kwahiyo sasa wanakwenda tarehe 30 (vs Simba SC), jana tulikuwa kambini kwao wakijiandaa na sisi tukawaambia Mtendaji Mkuu wetu Salaah Said Mohamed kasema kwamba hawa vijana kwa juhudi wanayoifanya akasema kwanini tusiwape Tsh. Milioni 30 wakishinda lakini ikitokea bahati mbaya wakaenda sare wapate Tsh. Milioni 10”

Silent Ocean ni Wadhamini Wakuu wa Tanzania Prisons na wamekuwa na utamaduni wakuwapa motisha Wachezaji wanapocheza mechi, mechi yao dhidi ya Yanga SC walipewa ahadi ya Tsh. Milioni 20 kama wangeifunga na Tsh. Milioni 10 kama wangetoka sare.
Screenshot_20221229_054134_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali imesema itaendelea kutekeleza sera yake ya kuunganisha Mkoa kwa Mkoa na Wilaya kwa Wilaya kwa Barabara za lami ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria, mazao na malighafi mbalimbali ili kukuza uchumi kwa haraka.

Akizungumza Wilayani Kyela Mkoani Mbeya wakati wa utiaji saini mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Ibanda hadi Kajunjumele (KM 22), Kajunjumele hadi Kiwira Port (KM 6) na Kajunjumele hadi Itungi Port (KM 4) Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kukamilika kwa Barabara hizo kutaimarisha shughuli za kiuchumi kwa Wakazi wa Wilaya za Rungwe na Kyela, na Mikoa ya Ruvuma, Njombe na nchi jirani ya Malawi.

“Katika ukanda huu kuna malighafi na mazao ya kilimo, uvuvi na makaa ya mawe mengi yanayohitaji miundombinu rafiki kwa ajili ya kuwafikia watumiaji kwa wakati, ndio maana Serikali ya awamu ya sita imeamua kujenga Barabara hizi kwa pamoja”

Waziri Prof. Mbarawa amewataka Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kumsimamia vizuri Mkandarasi anayejenga Barabara hiyo ili azingatie viwango na thamani ya fedha kulingana na mikataba “TANROADS itafanya uthamini upya ili kuhakikisha Wananchi wanaopisha ujenzi wa Barabara hizo wanapata stahili zao kwa mujibu wa sheria”
Screenshot_20221229_054226_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali kupitia Wizara ya Afya inatarajia kuja na mwongozo wa gharama za matibabu katika Vituo vya kutolea huduma za Afya vya umma nchini ambao unatarajiwa kuanza kutumika kuanzia mwezi Februari 2023.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu @ummymwalimu alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke kuona hali ya utoaji huduma za afya pamoja na kusikiliza kero, ushauri na maoni ya wananchi juu ya upatikanaji wa huduma za afya nchini.

“Kero ya Watu wengi hapa ni gharama za matibabu, tumepokea maoni ya Wananchi, Hospitali zetu wamejiwekea gharama bila hata kupewa mwongozo, sasa hivi Wizara inakamilisha Mwongozo wa uchangiaji gharama za matibabu na utaanza kutumika mwezi February 2023”

Waziri Ummy amesema kuwa Sera ya Afya ya Mwaka 2007 inaelekeza Wananchi kuchangia gharama za matibabu hivyo kupitia mwongozo huo utatoa mchanganuo wa gharama za kumuona Daktari kuanzia ngazi ya Zahanati, Vituo Vya Afya, Hospitali ya Rufaa, Wilaya, Mkoa, Kanda, Maalum na Taifa.

Waziri Ummy amesema hapo awali hakukuwa na mwongozo unaoainisha gharama husika za kumuona daktari hivyo kupelea vituo vingi vya kutoa huduma za afya kuwa na gharama tofauti tofauti zisizoendana hivyo kuleta kero zaidi kwa Wananchi.
Screenshot_20221229_054627_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom