Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (Sua), Dk Felix Nandonde amesema kuanzishwa kwa kiwanda cha sukari Bagamoyo, Mkoa wa Pwani ni jambo kubwa ambalo litasaidia kupunguza uhaba wa sukari nchini.
Dk Nandonde amebainisha hayo leo Jumatano, Desemba 28, 2022 wakati akichangia mjadala kuhusu matukuo ya mwaka 2022 katika Mwananchi Twitter Space.
"Kwa sasa Bagamoyo Sugar wanazalisha tani 30,000 lakini kufikia mwaka 2030 watafikia tani 100,000. Wameanza vizuri kwenye hili na matumaini ni makubwa siku zijazo," amesema Dk Nandonde.
"Serikali inatengeneza mazingira wezeshi na moja ya mambo ambayo wafanyabiashara wanahitaji ni maeneo ya kufanyia biashara. Hili linawezekana tukalipatia dawa," amesema Dk Nandonde.