Makapuku Forum

DEAL DONE:
KAYEMBE
NAMUNGO FC
.
Klabu ya Namungo imefanikiwa kuinasa saini ya Mshambuliaji wa Kimataifa wa Congo, Alidor Kayembe kwa mkataba wa Miaka miwili.
.
Kayembe (24) msimu uliopita amechukua Ubingwa akiwa na Red Arrows ya Zambia.
 
OFFICIAL: Chris Kope Mugalu
amejiunga na Klabu ya Al-Quwa Al-Jawiya iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Iraq

.
Ikumbukwe Lamine Moro pia anakipiga kwa sasa katika timu ya Newroz SC ya Iraq.
 
Hizi hapa Klabu 5 Bora Ukanda wa CECAFA
.
1. Simba SC — 14

2. Al Hilal Omdurman — 19

3. Al Merrikh — 31

4. Gor Mahia — 41

5. Namungo — 56

5. KCCA — 56

5. Rayon — 56

.
Chama lako namba ngapi …!
 
NINJA KUTIMKIA GEITA GOLD

.
Beki wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ anajiandaa kutua Geita Gold baada ya klabu hiyo ya Geita kumuomba kwa Mkopo ili akaiongezee nguvu safu yake ya ulinzi na uzoefu wake utasaidia kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
.
Ninja amethibitisha taarifa hiyo, amekiri kupokea ofa ya Geita Gold na kwamba alikubaliana nao na sasa ameuomba uongozi wa Yanga umwachie kwa mkopo.

………..
 
| KOTEI ATIMKIA MTIBWA SUGAR

.
Kiungo wa Singida Big Stars, James Kotei
amekamilisha kujiunga na Mtibwa Sugar kwa mkopo wa mwaka mmoja.
.
Kotei ambaye aliwahi kuichezea Simba licha ya kujiunga na Mtibwa, hivi karibuni alisaini mkataba wa miaka miwili na Singida.

………………….
 
CHELSEA BADO KIDOGO TU KWA DE JONG
.
Lisemwalo ni kwamba Chelsea inaelekea kushinda vita ya kufukuzia huduma ya kiungo Frenkie de Jong baada ya miamba hiyo ya Stamford Bridge kuwa kwenye hatua za mwisho kukubaliana na Barcelona juu ya dili la Pauni 67.6 milioni.
.
Taarifa hizo zitapokewa kama pigo kubwa kwa Manchester United ambayo ilimworodhesha kiungo huyo kuwa chaguo lao la kwanza kwenye usajili wa dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya.
.
Licha ya De Jong,25, kudai kwamba hataki kuondoka Nou Camp, Barca wao wanachokifanya ni kumlazimisha kuhama.

…………
 
Fafhan Jr

Sheikh Ally ngoja tuongee kitu My Brother, tusiongee kama Mwandishi na Rais wa Yanga, bali tuongee kama Braza na mdogo wake, ngoja nikuelekeze kitu tena chepesi sana

Kama una kalamu hapo karibu basi andika jina la ANAS LAGHRARI moja kati ya vichwa na Mastermind nyuma ya European Superleague (siku moja nitaelezea, watu hawamfahamu kabisa) ana umri mdogo wa miaka 37 hii ndio Injini ya Perez, Rais wa Real Madrid ni watu wa karibu mno.

Jioni moja baada ya European Superleague kufeli, Kijana Laghrari wakati yupo na Perez kwenye mgahawa mmoja jijini Madrid akamuuliza “President tayari FIFA wamekugeuka, UEFA wamechukizwa na La Liga hawataki kukusikia, utaishije na timu yako?” Lilikuwa swali kwa Perez

Perez akapiga fundo moja kwanza la wine kisha akamwambia “Kijana wangu mdogo, hakuna kitu chochote ambacho FIFA au UEFA wanaweza kuipa Real Madrid na hakuna tatizo lolote mimi nisipokuwa karibu na wao” akaweka nukta kisha akaendelea

“Nachopaswa kukifanya kama Perez ni kuwekeza sana kwenye timu, kusajili vizuri na kubeba makombe na hiyo ndio njia pekee ya kuwakumbusha juu ya uwepo wangu na uwepo wa Real Madrid” akamaliza kisha akamtazama tena Laghrari

“Kwenye hii dunia ya mpira Kijana wangu kinachodumu ni mafanikio na historia, nitabeba makombe na kuweka historia, Rais wa FIFA atanipa mkono na Rais wa UEFA atanisalimia” akamaliza Rais Perez

Sheikh Ally umeipata hiyo historia? Umeelewa maana yangu? Well maana yangu ni kuwa una kazi mezani, una kazi ya kuhakikisha Yanga inazidi kuwa bora, endelea kubeba makombe, endelea kuonesha utofauti, watu watakuja mezani

Huu sio muda wa kulalamikia chochote, kujuta kwa chochote bali ni muda wa kuisuka upya ndoto ya Wananchi, kurekebisha panavuja na kuwapeleka Wananchi nchi ya ahadi, ndio jukumu ambalo unalo mikononi, ingia ofisini ongoza njia

In football its all about merit, you know the way Bro
GOD BLESS YOU
 
“Sijajua kwanini mjadala huwa unakuja inapotokea timu za Afrika wakati ni masaa sita tu kutoka Ulaya hadi hapa ila ni masaa 18 kutoka Ulaya mpaka Brazil ila husikii kelele, bendera ya taifa ina muhimu kuliko klabu” Kocha Aliou Cisse, kuhusu kauli ya mmliki wa Napoli
 
Rasmi Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli ameaga uongozi na mashabiki wa timu hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram na ameshukuru kwa nafasi aliyopewa kutumikia Wananchi. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mpito wa Yanga, Wakili Simon Patrick alisema mkataba wa Bumbuli umemalizika na nafasi yake tayari imetangazwa kwa ajili ya kupata mtu mwingine.
 
UONGOZI wa Yanga umetoa kauli juu ya kutoalikwa katika Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), bado hawajajua sababu za kutopewa mualiko.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga wakili Simon Patrick akizungumza na kituo cha radio cha E-fm amesema wamelazimika kufuatilia mkutano huo kupitia mitandao baada ya kutopata mualiko.

Simon amesema Yanga ambao ni mabingwa wa nchi walitamani kuwepo katika mkutano huo unaonendelea jijini Arusha na kuhudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

"Bahati mbaya hatujajua kipi kimetokea na sisi (Yanga) kukosa mualiko, tuliamua kutumia fursa ya teknolojia tuweze kufuatilia mkutano huu,"amesema Simon.

"Ni jambo jema tunafurahi limerfanyika hapa Tanzania, kwa manufaa mapana ya nchi yetu wamepata kutangaza utalii, wamepata kujionea mazuri ya Tanzania."
 
Wakimwelezea Ki kwa nyakati tofauti, mastaa wa zamani, beki Williams Mtendamema aliliambia Mwanaspoti Aziz Ki ni fundi atakayesaidiana na Mayele kuzalisha mabao mengi, isipokuwa kwa sasa anatakiwa kuyazoea mazingira kwa haraka.

Ki ambaye usajili wake ulitikisa Yanga ikimsajili kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast kiwango alichokionyesha dhidi ya Vipers ya Uganda ndicho kilichomfanya Mtendamema kumchambua kiufundi.

“Mashabiki wanapaswa kumpa muda, ni mchezaji mzuri sana, wasitarajie mechi moja tu anafanya makubwa, kuna kuzoea mazingira na bado kocha anatengeneza kombinesheni,” alisema na kuongeza;

“Wachezaji wa Yanga walionyesha uwezo wa mchezaji mmoja mmoja siyo kitimu walipocheza na Vipers lakini wengi wanajua mpira, ukiachana na Ki yupo Gael Bigirimana jamaa haimbwi ila atakuja kuwashangaza wengi.”

Mchezaji mwingine wa zamani wa timu hiyo, Andrew Tito alisema kupitia tamasha la Wiki ya Mwananchi, ameona ufundi wa mastaa, anaamini baada ya mechi tatu za Ligi Kuu Bara ikianza Agosti 15 watafanya makubwa.

“Kikosi cha Yanga kina wachezaji watulivu wanaotumia akili kubwa, ukiachana na waliyokuwepo na timu msimu uliyoisha, hawa wapya wameongeza nguvu mfano Ki na Bigirimana,” alisema.

 
KIUNGO mpya wa Simba, Nelson Okwa amewaambia Yanga, “bado nyie.” Staa huyo ametuma salamu kwa watani zao akisema kile alichoonyesha kwenye kilele cha tamasha la Simba Day juzi Jumatatu ni mfano tu.

Katika tamasha hilo, Simba ilicheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Ethiopia, St George ambapo ilishinda mabao 2-0 huku moja likifungwa na nyota huyo raia wa Nigeria.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Okwa alionyesha kiwango bora hasa mikimbio na pasi za haraka haraka.

Akizungumza na Mwanaspoti, Okwa alisema: “Nilichoonyesha ni mfano tu kwa mashabiki wa Simba. Nadhani nitakuwa kwenye kiwango bora muda si mrefu ligi ikianza hadi mwisho wa msimu,”
 
KIUNGO Hassan Dilunga ameamua kuvunja ukimya baada ya kutokea sintofahamu ya kutotambulishwa katika Tamasha la Simba Day.

Gazeti mama la (Mwananchi) liliwahi kumkariri Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu akisema Dilunga bado ni mchezaji wao na yupo kwenye matibabu, ingwa si kati ya waliotangazwa kuachwa au kuagwa rasmi kama ilivyokuwa kwa Tadeo Lwanga, Cris Mugalu na Meddie Kagere.

Mwanaspoti lilimtafuta Dilunga na alisema mkataba wake umeisha (Umebakiza siku chache) na bado hajasaini mkataba mpya na timu hiyo lakini bosi (Jina kapuni) alisema atamtafuta.

“Upande wa afya yangu naendelea vizuri lakini kurudi uwanjani ni Januari Mungu akipenda,” alisema Dilunga ambaye aliumia goti na kushindwa kumalizia msimu na alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…