Imeandikwa na @swalehmawele
FT: Simba SC 2-0 ST. George.
Simba SC wamehitimisha sherehe zao za Simba day kwa ushindi, performance nzuri hasa katika kipindi cha pili, kipindi cha kwanza timu iliweka lock mbele na ikawa haitengenezi nafasi za kutosha, ilikuwa rahisi kwa St George kuzuia kwa sababu mikimbio mingi ilifanywa katika zone ya pili.
Okrah, Kibu na Sakho wote ni wachezaji ambao aina yao ya uchezaji inafanana, wanapenda kukimbia na mpira muda wote hasa kutokea pembeni ( inverted ), athari yake Simba ikakosa mtu ambae anaweza ku control timu katikati ( zonal 14 ) kitu ambacho kingefungua mianya kwenye kushambulia.
St. George imewapa picha Simba SC ni namna gani wanaweza kuzipa njia wanapofanyiwa transition, wameonyesha uthubutu wa kucheza na kutengeneza nafasi za kufunga, bahati njema zipo nyakati ambazo walikutana na Benno Kakokanya aliekuwepo kazini, mwamba anaulizia nafasi yake kwa benchi la ufundi.
Mohammed Ouattara, ameonyesha kitu katika dakika tisini alizozicheza, mgumu, mzuri akiwa na mpira na uwezo wa kucheza mipira ya juu na kuanzisha mashambulizi kutokea chini, muda wote anafikiria ni vipi timu itasogea juu.
Yule Gattouch Panom wa Ethiopia mtu wa kazi sana, mtulivu na mzuri katika kuzuia, kiungo mgumu.
Vitu vya Chama hufanywa na Chama mwenyewe, what a player, sehemu ambayo unahisi atapiga yeye atafinya, si rahisi kufanya alichokifanya leo.
Kama Zoran atakuwa anatumia 4-2-3-1 nadhani Jonas Mkude ni mchezaji muhimu, naiona partnership yake na Vicent Akpan.