Kwa yanayoendelea hadi sasa Ni Bora tukumbushane . Tanzania msimu ujao itawakilishwa na klabu nne, zikiwamo Simba na Yanga huko klabu bingwa na Geita na Azam zitakazokinukisha kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
.
Matumaini makubwa ya wadau wa soka wameyawekwa kwa Simba na Yanga Hata hivyo, katikati ya tumaini hilo la wadau wa soka, ni wazi vigogo hivyo lazima vijipange kwelikweli msimu ujao kwani wasipofanyaa hivyo huenda hata hatua ya makundi waisikie tu hewani.
.
Afisa Habari wa Yanga SC hayupo kwenye Kamati ya maandalizi ya Wiki ya Mwananchi, kisha kuna Mwandishi mwingine mkongwe kawekwa.
Hiki sio kitu cha kawaida kwenye maandalizi ya mashindano na matamasha, media officer wa taasisi umuhimu wake ni wazi kabisa, vinginevyo hujui hayo mambo au mmeamua kumuondoa na kumleta mtu wenu.
Saa chache baada ya uongozi wa Yanga kutangaza kwamba aliyekuwa Ofisa Mtendaji wao Mkuu Senzo Mazingiza anaondoka mwenyewe ameibuka na kukanusha juu ya kuondoka kwake kuhusishwa na ujio wa mshambuliaji Bernard Morrison.
Akizungumzia ishu ya kupishana mara mbili na kiungo mshambuliaji Bernard Morrison Senzo amesema wala hana tatizo na usajili huo na kwamba alihusika mara zote kumsajili Mghana huyo katika klabu zote.
"Niliwahi kuwaambia ninyi Mwanaspoti juu ya Morrison, bahati mbaya hapa Tanzania uongo hupewa nafasi kubwa kusambaa, nilisema nilipokuwa Simba nilihusika kumleta Morrison pale lakini bahati mbaya wakati anafika mimi nilikuwa naondoka," amesema Senzo
"Nikiwa hapa Yanga pia imekuwa hivyohivyo, viongozi wenzangu wanajua jinsi tulivyoshirikiana kumleta huyu Morrison, huyu ni mchezaji bora bila kuangalia mambo yake yanayosemwa.
Wakati dirisha la maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2022/2023 likiwa wazi kwa muda wa siku 70 kuanzia Julai 19 hadi Septemba 30 mwaka huu, Serikali imetangaza Tume ya Watu watatu kuchunguza utoaji wa mikopo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Tume hiyo itaongozwa na Prof Allan Mushi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, Idd Makame kutoka Zanzibar na Dkt Martin Chegeni ambao wote kwa pamoja ni Wataalamu wa mifumo waliobobea katika sayansi ya Kompyuta na Takwimu.
Tume hiyo itachunguza uhalali katika utoaji wa mikopo kwa Wanafunzi wa elimu ya juu kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2017/2018 mpaka 2021/2022 ili kubaini kama kulikuwa na upendeleo kwa Watu wasiokuwa na sifa.
Waziri Mkenda amesema kuwa Tume hiyo itapitia malalamiko ya Wanafunzi mbalimbali nchini ambao wamekuwa wakiyatoa kuhusu upendeleo wa utoaji mikopo kwa kupata mikopo kwa Wanafunzi wenye sifa huku wale wasiokuwa na sifa stahiki wakikosa mikopo hiyo.
“Na kwenye hili tunakaribisha Watu watoe taarifa kwasababu kama kuna Mtoto wa Mkenda uliyesoma nae utakuwa unamjua Baba yake ni nani na uwezo wake, halafu wewe unaona Mtu huyo amepewa mkopo toa taarifa”
Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally akiizungumza leo Dar es salaam kwenye uzinduzi wa Wiki ya Simba amesema “Kesho mtajua tofauti ya Mdhamini na msaada, tutakuwa na tukio na Mdhamini wetu mpya, kampuni ya M-Bet”
“Wachezaji ambao tunawasajili sio wa sandakalawe, ni Wachezaji muhimu kwenye vikosi vyao hivyo kunakuwa na ugumu kuwapata, inabidi kuzungumza na vilabu vyao ili kuwashawishi”
CEO wa Simba, Barbara Gonzalez akizungumza leo Dar es salaam kwenye sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Simba amesema “Zoezi la usajili bado linaendelea, Wiki ijayo Timu yetu ya digital itaanza kutangaza Wachezaji wengine”
“Leo ni uzinduzi rasmi wa Simba Week, tuna mambo mengi kwenye Wiki hii, Msimu huu tunarudi kwa nguvu, tunarudi kutetea ubingwa wetu na slogan yetu ni WE ARE UNSTOPPABLE - HATUSHIKIKI – HATUZUILIKI”
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu akizungumza na Mashabiki wa Simba kwenye sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Simba leo Dar es salaam ameomba radhi Mashabiki kwa Klabu hiyo kutokufanya vizuri msimu uliopita.
“Tunaomba radhi kwa msimu uliopita lakini ilikuwa ni funzo, tunafanya kazi kuhakikisha tunafanya usajili mzuri ili tusisimamishwe na Mtu yeyote, tumejipanga kuwa na msimu bora zaidi”
“Nawahakikishia tupo vizuri na tutaendelea kuwa vizuri”
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu akizungumza na Mashabiki wa Simba kwenye sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Simba leo Dar es salaam amesema jezi za Klabu hiyo msimu huu zinatoka Ulaya na sio China na zitazinduliwa Wiki hii.
“Kuhusu jezi msimu huu tumeacha kwenda kule hung haa (China), sasa jezi zetu zinatoka Ulaya, hazitoki tena Asia, Wiki hii tunazindua”
“Kwanza niseme Simba usajili hatujamaliza, sasa taarifa rasmi kuhusu usajili wa Simba nenda kwenye platforms za Simba, najua CEO wiki hii ataachia kitu."
"Simba ndio tumekuwa wa kwanza kuanzisha mambo makubwa, acha wengine waige mambo yetu mazuri, sisi hatutaiga mambo yao mabaya”
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara kuchukua nafasi ya Dk Raphael Chegeni ameya uteuzi wake umetenguliwa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.