Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ameagiza kusimamishwa kazi na kuhojiwa na Taasisi Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) watumishi watano kutokana kuisababishia hasara Halmashauri ya Wilaya Kiteto Mkoani Manyara.
Bashungwa amesema “Ukifanya ubadhilifu na kuhamia Halmashauri nyingine au Taasisi yoyote ya Serikali, nitakufuata huko huko niseme na wewe, bora kufia site kuliko kumuangusha Rais wetu Samia Suluhu Hassan”
Watumishi hao ni aliyekuwa Mweka Hazina, Nassoro Mkwanda na Mhasibu wa Mapato, Christopher Mwigani, Kaimu Mwanasheria wa Halmashauri Joseph J. Hoza, Kaimu Mweka Hazina Hadija Boffu pamoja na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi Nakaji Mollel.
Kati ya hao ni Nassoro Mkwanda aliyehamishiwa Mafinga Mji, Khadija Bofu aliyehamishiwa Songea Manispaa na Christopher Mwigani ambaye amestaafu, wote wanatuhumia kuhamisha fedha na kuweka kwenye akaunti ya amana isiyo na vifungu vya matumuzi na wanatakiwa kurejeshwa kwenye Halmashauri hiyi kujibu tuhuma hizo.
Pia Kaimu Mkuu wa kitengo cha manunuzi Nakaji Melateki Mollel ambaye aliidhinisha Sh milioni 191.9 kwa ajili ya kununua vifaa vya ujenzi bila kufauta taratibu sambamba na Sh milioni 235.5 alizolipa mkandarasi wa kuchimbia visima bila kuzifanyiwa tathimini na Khalfan Hinga aliyetoa kazi hiyo bila kufanyika tathimini.