[emoji3578][emoji3578] Jemedari Said
KUNA MAHALI LIPO TATIZO SIO BURE...Part 2
Mhamasishaji alikataa kwamba kwenye mzozo wake na Rais wa TFF hakukuwa na MATUSI...!!
Akaja akaomba radhi kwa kumkosea Rais wa TFF na mpira kwa jumla.
Leo anakiri kulikuwa na MATUSI anaposema Rais wa TFF aliongea maneno mabaya alisema " Watu wa Yanga wote wana vinyesi sehemu za siri muda huu" Haya sio matusi?
Jamii inapaswa kumjua mtu huyu kama TATIZO KUU kwenye mpira wetu. Huwa anabadili badili maneno kwa faida yake. Huwa anatatafuta sana huruma kwa manufaa yake.
Leo anahusisha VAGI lake lile na Yanga, kwani Yanga ndo walimtuma akafanye fujo? Leo anasema kuhusu siku ya Mwananchi, yeye alikuwa Simba na Yanga walifanya Siku ya Mwananchi Bora kuliko Simba Day ambayo yeye alishiriki. Yanga wanaweza kufanya jambo lao bila msaada wa MAMLUKI kutoka Simba.
Anataka huruma kwa Serikali pale anaposema aliandaa ujumbe kwajili ya SENSA 2022, huo ujumbe si wa Yanga sio wake, Yanga sio yeye ni Taasisi, yeye atumikie KIFUNGO Yanga ina watu wengi watafikisha ujumbe kwa Serikali yeye akiwa jukwaani au nyumbani akiangalia kwa TV hakun'shaka.
Huyu jamaa ni tatizo sana, anataja kuonyesha kwamba yeye ana nguvu na kufungiwa ni shida kwenye mpira au anataka NCHI ISITAWALIKE kisa yeye kufungiwa, yeye nani kwani?
Anasema Serikali iingilie kati anaonewa, lakini anasema Waziri alitoa hukumu kwenye hotuba yake siku ya Tuzo. Nadhani pia Serikali iwe makini na ianze kumfatilia mtu huyu anajiona kuwa juu ya mamlaka zinazomuongoza.
Kila siku yeye ndo press conference kaonewa, kaomba msamaha, Yanga inaonewa, Barbara anamuonea, MO Dewji hampendi, huyu jamaa ni tatizo na hajijui kama ni shida.
Kamati kusema kuhusu packet ya cigarette kibiriti cha gas kuna shida gani kwani unavuta kwa siri familia haijui mpaka useme unadharirishwa?
Maneno haya dhidi ya Rais wa TFF nia nini kwamba Rais atoke mafichoni ajibu? Kwanini yasingesubiri Kamati ya Rufaa ya Maadili au hukati tena?
NB: Ukicheka na Mbwa utaingia nae Msikitini.