Usafi kwa wanyama unapimwa kutokana na namna mfumo, tabia na utaratibu mzima wa maisha yao ya kila siku, tunapochanganya ni tunampima kutokana na namna sisi binadamu tunavyo rank' usafi kwa namna yetu.
Ukiachana na hilo usafi unachukua nafasi zaidi kwenye mpangilio sahihi na kuweka kila kitu kinapostahili (Bila kusahau kua na mwili safi na mavazi safi kwetu binadamu), mfano mdogo kuna watu ambao wana nguo za kila namna lakini bado unamuona sio msafi pengine hazingatii kuzisafisha vizuri na kuzipangilia kuliko yule ambae ana nguo chache lakini anazingatia mpangilio kwamba avae nini na wakati gani.
Kwa Nguruwe wana utaratibu wao ambao ni nadra sana kukuta kwa wanyama wengine ambao ni kutenga sehemu maalumu ya kujisaidia na kulala, na ni nadra kukuta amejisaidia sehemu ambayo huwa analala.
Wanapenda zaidi baridi sababu hawana tezi jasho hivyo kukiwa na joto kali huwa wanapata tabu, ili kupunguza joto hulazimika kujipaka matope na kujimwagia maji (Kimuonekano sisi tunamuona mchafu lakini kwao ndio kuoga, hii hata Tembo hufanya sana).
Unaweza kufanya utafiti, ukiwa na Nguruwe hakikisha unazingatia usafi, mpe chakula kwa wakati, hakikisha banda lake lipo kwenye hali ya ubaridi zaidi. Kwa muda wote atakua mwenye muonekano wa usafi kama ambavyo unataka