Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,167
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), linatoa pole kwa Familia ya marehemu Ngaitepa Marias Lukumay (17) mkazi wa kijiji cha Pangaro Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro kwa kumpoteza kijana wao kutokana na mvutano uliotokea kati ya Askari wa Hifadhi na Wananchi baada ya mifugo ya Wananchi kukamatwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Mkomazi Julai 5, 2022.
Shirika kwa upande wake limesema limeanza kulifanyia uchunguzi wa kina tukio hilo ili kuhakikisha kuwa mahusiano mazuri kati ya wananchi na hifadhi yanaendelea kuwapo kama kawaida.
Aidha, Shirika limesema litaendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi wanaoishi kandokando ya hifadhi kupitia Mradi wa Ujirani Mwema kuhusiana na Sheria za Hifadhi za Taifa na taratibu za kufuatwa kwa wanaokiuka ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya maeneo ya Hifadhi za Taifa ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kunapokuwa na mvutano usiofuata taratibu za kisheria.