Makapuku Forum

Makapuku Forum

[emoji954] MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI LIGI KUU YA WANAWAKE - CLARA LUVANGA (Yanga Princess)
Screenshot_20220708-042727_OGInsta%2B.jpg
 
Mchezaji wa Geita FC George Mpole ambaye ndio Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania bara 2021/2022 amesema swala lake la kukosekana kwenye orodha ya wanaowania Tuzo za NBC TFF zinazotolewa usiku huu anamuachia Mungu na kusisitiza "siwezi kuongelea lolote nadhani Wananchi na Watanzania wameona kila kitu kwahiyo mambo mengine tunamuachia Mwenyenzi Mungu yeye ndiye anaejua"

Mchezaji wa Geita FC George Mpole amelijibu swali ambalo wengi wamekua wakitamani kupata jibu kutoka kwake kama msimu ujao atahamia kwenye Club kubwa za Dar es salaam ambazo ni Yanga, Simba na Azam FC.

Kwenye mahojiano na Azam Sports 2 kwenye red carpert ya Tuzo za TFF 2022, Mpole amesema kwa sasa hawezi kusema chochote mpaka muda utakapofika na kila kitu kitakuwa wazi, namnukuu akisema "tusubiri muda, muda utaongea kila kitu kitakuwa wazi"
Screenshot_20220708-043840_OGInsta%2B.jpg
 
Kipa wa Simba SC Aishi Manula @28_manula amesema ni kweli Watanzania wengi wanatamani aende kucheza soka nje ya Tanzania lakini changamoto ni kwamba hajapata Club anazozitaka.

"Wengi hawafahamu, wengi wanakwambia tu wanatamani kuona umeenda nje lakini bila kujali umeenda nje ya wapi, sisi Makipa tuna mipaka, zile Nchi za Kiarabu hasa wale Waarabu weupe hawawezi kuchukua Kipa kutoka nje ya Nchi kwahiyo ili utoke Tanzania kuna Nchi kadhaa tu ambazo umewekewa Congo, South Africa, Angola na kwengine ambayo leo hii Ligi yetu ya Tanzania ni kubwa, wote wanatamani kucheza Tanzania"

"Muda mwingine napata ofa, napata Timu wakati mwingine napata timu ambayo ni kubwa, ya average ambayo haishiriki michuano ya kimataifa lakini mimi lengo langu ni kushiriki michuano ya kimataifa ili nipate platfoarm zaidi.... muda mwingine natamani kwenda nje lakini kulingana na nikiangalia nataka kucheza Champions league, Confederation cup kwahiyo kuna mambo mengi ambayo yananikabili ambayo Watanzania hawayaangalii wao wananitaka tu niende nje" ——— amesema Aishi Manula.
Screenshot_20220708-044134_OGInsta%2B.jpg
 
Rwanda na Congo zimekubaliana kupunguza mzozo baada ya kufanya mazungumzo ya siku moja yaliyoongozwa na Angola kati ya Marais Paul Kagame na Felix Tshisekedi ambapo mataifa hayo mawili yataifufua Tume ya Congo na Rwanda itakayoanza tena kazi July 12 katika Mji Mkuu wa Angola, Luanda.

Mazungumzo haya pia yametaka kurejeshwa kwa uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Congo DRC, usitishwaji wa uhasama na kuondolewa mara moja kwa Waasi wa M23 kutoka kwenye ngome zake mashariki mwa Congo.

Baada ya mazungumzo haya Rais Paul Kagame amesema "Namshukuru Rais Tshisedeki kwa michango yake inayotuwezesha nasi kuchangia ili mambo yasonge mbele, tunatarajia kurejesha mahusiano ya Nchi zetu katika hali ya kawaida"

Naye Rais Tshisekedi amesema anaamini mchakato huu utahitimisha haraka uhasama na mapigano na kurejesha utulivu kwenye mataifa hayo ambapo Umoja wa Afrika mwaka huu uliiomba Angola kuwa Mpatanishi wa Nchi hizi ili kumaliza mzozo huu ambao umesababisha Watu zaidi ya laki moja na elfu 70 kupoteza makazi yao tangu Kundi la M23 lilipoibuka tena Congo.
Screenshot_20220708-044329_OGInsta%2B.jpg
 
Siku chache baada ya @ayotv_ kuripoti tukio la mauaji ya kijana Ibrahimu Nicodems mkazi wa Sawe Babati kuuawa kwa kuchomwa kisu na Thomas Amsii (Binamu yake) na Mtuhumiwa huyo kuachiwa kwa dhamana, Wananchi wa eneo hilo wameandamana wakitaka Mtuhumiwa achukuliwe hatua.

Taharuki hiyo imemlazimu Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange kufika Sawe na kuzungumza na Wananchi hao ambao walalamika Mtuhumiwa kuachiwa.

DC amesema “Kwa maelezo niliyoyasikia hapa nimegundua zoezi hili limepelekwa harakaharaka, bado Mimi nalia na upelelzi ulitakiwa uende mbali zaidi kujiridhisha, Wapelelezi wangu mna matatizo kadhaa, kuna Mtu ana kesi ya ng'ombe anabishana na mwenzake umemuweka ndani kwa siku 52 lakini hapa pana kesi Mtu kafa hata wiki haijaisha yupo nje, hapana haiwezekani"

DC Twange ameagiza kila aliyehusika kukamatwa leo ikiwemo waliotoa barua za kuomba dhamana pamoja na Mashahidi walioenda kuwaombea dhamana.
Screenshot_20220708-044424_OGInsta%2B.jpg
 
Mbunge wa Nzega Vijijini na Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Dr. Hamis Kigwagalla amesema alipata miaka mitano ya kuhudumu Serikalini, ni mingi na anayo mengi ya kuonesha na wala hana majuto mengi moyoni.

“Nilipata miaka mitano ya kuhudumu Serikalini, ni mingi na nina mengi ya kuonesha, sina majuto mengi moyoni, niliiitendeq haki nafasi niliyopewa kutoa mchango wangu kwa nchi yetu! acha niendelee kulihudumia jimbo letu tu kwa sasa”

Kigwangalla ameyasema haya akimjibu Mtu aliyemuandikia yafuatayo kwenye ukurasa wa twitter “Una uwezo mkubwa saana Mheshimiwa kwenye kufikiri na kiutendaji, sema muda na mfumo itabaki kuwa changamoto kwako ..
Screenshot_20220708-045029_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson ametangaza kujiuzulu kama Kiongozi wa Chama cha Conservative kufuatia wimbi la kujiuzulu kwa Serikali.

Boris amesema “Ni wazi sasa ni mapenzi ya Chama cha Wabunge cha Conservative kwamba kuwe na Kiongosi mpya wa Chama hiki na Waziri Mkuu mpya, nataka kusema kwa mamilioni ya watu ambao walitupigia kura mwaka wa 2019, wengi wao walipiga kura ya Conservative, kwa mara ya kwanza, asante kwa mamlaka hayo mlionipa na kwa Conservative wengi, tangu 1987”

Siku ya jana Johnson alisema kuwa atabaki na kupigania nafasi yake lakini orodha ya kujiuzulu kwa Mawaziri wa Serikali iliendelea hadi kufikia leo ambapo jumla ya Mawaziri waliojiuzulu imefikia 58 kufuatia barua nyingi za Mawaziri hao zikimkosoa Boris aliyekumbwa na kashfa na kumtaka ajiuzulu nafasi hiyo ya kuwa Waziri Mkuu.

Kwa sasa Boris ataendelea kuhudumu kama Waziri Mkuu hadi October mwaka huu atakapopatikana Kiongozi mpya.
Screenshot_20220708-045154_OGInsta%2B.jpg
 
Tanzania na Afrika Kusini zimesaini makubaliano ya Kiswahili kufundishwa katika Shule za msingi za nchini Afrika Kusini.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda na Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini Angelina Motshekga wamesaini hati za makubaliano hayo mbele ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango katika maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani yanayofanyika Dar es salaam.
Screenshot_20220708-045308_OGInsta%2B.jpg
 
Kwa mara ya kwanza toka enzi leo July 7 2022 dunia inaadhimisha siku ya Kiswahili duniani ambayo iliidhinishwa na UNESCO, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni ambalo pia ni Wakala maalumu wa Umoja wa Mataifa aliyelenga kukuza amani na usalama duniani kupitia ushirikiano wa kimataifa katika elimu, sanaa, sayansi na utamaduni.

Kiswahili kimefika na kinafundishwa katika Nchi mbalimbali duniani ikiwemo China ambako Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki amesema Chuo Kikuu cha China cha Mawasiliano ya Habari ni miongoni mwa walioadhimisha siku hii kwa ukubwa wake na kutuma salamu kwa kutumia kiswahili.

November mwaka 2021 UNESCO walitangaza July 7 kuwa siku ya Kiswahili duniani ambapo mwaka huu ndio mara ya kwanza maadhimisho yake kufanyika.
Screenshot_20220708-050014_OGInsta%2B.jpg
 
Mwimbaji staa wa R&B Robert Sylvester Kelly maarufu R. Kelly ambaye hivi juzi amehukumiwa kwenda jela kwa miaka 30, ameondolewa kwenye uangalizi maalum aliokua amewekwa gerezani kumuepusha kujiua.

Imeelezwa kwamba R.Kelly aliwekwa kwenye uangalizi huo kutokana na kuwa kwenye hatari ya kutaka kujiua kutokana na msongo wa mawazo uliotokana na mashtaka ya kuwadhalilisha kingono Wanawake na Wasichana yaliyopelekea ahukumiwe kifungo cha miaka 30 katika gereza la Brooklyn, New York.

Waendesha mashtaka hapo awali walisema Mwimbaji huyu mwenye umri wa miaka 55 alihitajika kuwekwa kwenye uangalizi huu maalum kwasababu ya usalama wake lakini Mawakili wake walifungua kesi siku ya Ijumaa wakidai aliwekwa kwenye lindo hilo maalum kama adhabu na sio kusaidiwa.

Uangalizi huu maalum maarufu ‘Suicide watch’ hufanywa kwa Mgonjwa au Mfungwa ambaye yupo katika hatari ya kujiua.
Screenshot_20220708-050106_OGInsta%2B.jpg
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga, Rodgers Gumbo ambaye anagombea nafasi ya ujumbe tena amesema baada ya kufanikisha kuyaleta makombe yote matatu sasa anataka kurudi tena kuhakikisha Yanga inafanya vyema katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Screenshot_20220708-050347_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom