Farhan Jr
Kuna muda Pablo anaongea maneno machungu sana pengine Viongozi au Mashabiki kama huyatafakari vyema unaweza kumchukia lakini wenzetu wapo hivyo, wanaishi kwenye neno UKWELI
Juzi juzi Rangnick alikuwa anawachana Bodi na wamiliki kuwa timu ipo chini haipo kwenye level za Liverpool, Chelsea wala Man City, kwake anaiona United ni timu ya kawaida tu sana
Ndivyo Pablo jana anakiri kuwa Pirates wapo mbali sana, sio kwa uwekezaji tu bali hata wachezaji, yeye kama Kocha kuna kitu atakuwa amekiona ambacho akisema Mwandishi inakuwa ngumu kueleweka
Ukinichukua Farhan kama Shabiki wa Simba naweza kuona kama Kocha anatuvua nguo, ila ukinichukua Farhan kama Mwandishi naona Mwalimu yupo sahihi tu sana, amezungumzia project kwa lugha ya kificho
Simba imepambana sana, nguvu inayotumika kufika robo ni kubwa sana, wachezaji wanajituma sana! Kiasi ambacho hakuna anaewadai
Ukweli ulio wazi sasa ni MO DEWJI kuilinda project, kama watauza wachezaji muhimu kila msimu itakuwa ngumu kuanza upya kila siku, kama tutaenda sokoni kupata wachezaji wengi kama INONGA that means kweli tutasogea Afrika
Hili tena sio suala la Kocha, Mashabiki wala wachezaji, reality check ni MO DEWJI sasa kuendelea kuweka pesa kweli kupata quality kubwa zaidi!
Nafurahi sana kumsikiliza Pablo kwenye interview zake, jana hakutumia muda kupiga kelele za VAR, yeye kazungumzia Mchezo kisha kagusa quality! MO DEWJI kazi kwako Kiongozi
Project ilindwe sana ipo siku Simba anaenda kufanya makubwa zaidi Afrika