Makapuku Forum

Makapuku Forum

Msanii staa wa Bongofleva Harmonize ametangaza ujio wa Afro East Carnival Season 2 ambayo itafanyika pale Uwanja wa Uhuru DSM siku May 29,2022.

Harmonize amesema atajitaidi kuwaleta Wasanii wengi alioshirikiana nao wa nje ya nchi ambao hawakuepo mara ya kwanza kwani changamoto kubwa waliyokutana nayo mwanzoni ni kushindwa kufanya mpango wa visa mapema.

Viingilio vya Tamash hilo vinaanzia Elfu 5 hadi Elfu 10 na kutakuwa pia na VIP.

"Sababu ya kufanya Season 2 DSM ni kwasababu naamini kuna Watu wengi hakuwagusa Kwenye Tamasha la kwanza hivyo nawaletea hili la pili ili mashabiki wangu wote wapate burudani na baada ya hapo itaenda mkoani"
Screenshot_20220422-200324_OGInsta%2B.jpg
 
Siku chache baada ya kuenea kwa video fupi zikionesha baadhi ya wauzaji wa dawa wakihojiwa na kuonesha kutokuwa na ujuzi wa dawa hizo, Baraza la Famasia Tanzania leo limepita mitaa ya Dar es salaam na kufanya ukaguzi ambapo wamebaini uwepo wa maduka bubu ambayo hayana vibali vya kuuza dawa na Wauzaji wake hawana taaluma na vyeti vinavyowaruhusu kuuza dawa "Tunayafungia maduka haya na Wamiliki na Wauzaji watachukuliwa hatua"

Ukaguzi huu uliofanywa na Maafisa kutoka Baraza la Famasaia wakiongozwa na Msajili wa Baraza hilo Elizabeth Shekalaghe, unakuja siku chache baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema ameziona video hizo na akaagiza Baraza hilo kutimiza wajibu wao kikamilifu ikiwemo kuchukua hatua maramoja na kuhakikisha maduka ya dawa yanaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni"

"Natoa rai kwa Watu wanapokwenda duka la dawa lazima wakute nembo lakini pia ukifika kwenye duka la dawa hakikisha unaona cheti cha mtoaji huduma" Elizabeth
Screenshot_20220422-200514_OGInsta%2B.jpg
 
Mbunge wa Jimbo la Mchinga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya nne, Salma Kikwete ameiomba Serikali kuwatengenezea mazingira mazuri wenza wa marais, makamu na mawaziri wakuu ili waweze kupata stahiki zao pindi wanapostaafu.

Akitoa hoja hiyo bungeni Dodoma, amesema kuwa mke wa Rais hutakiwa kustaafu kazi pindi mwenza wake anapoingia madarakani, hivyo kupoteza utaalamu wake wote, hivyo ni vyema apewe stahiki zake.

“Ninayaeleza haya kwa sababu mimi nilikuwa mke wa Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mimi ni mfano moja wapo, kuacha kazi si jambo baya ushauri wangu tengenezeni utaratibu wa kisheria ili tunapomaliza ule muda tujue tuna kitu gani tunachotakiwa tufanye," amesisitiza.
Screenshot_20220422-200705_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom