Makapuku Forum

Farhan Jr

PAPE OUSMAN SAKHO TRANSFER UPDATES


Utaratibu wa usajili ndani ya Simba sio tena wa mtu kati bali Agencies mbalimbali ambazo wanafanya nazo kazi, moja kati ya tip kubwa niliyonayo ni kuhusu POS

Kuna baadhi ya timu zinahitaji huduma yake barani Ulaya, kwenye nchi za Uturuki na Scandinavia wakihitaji haswa huduma ya Msenegal huyo anaekipiga Simba

Taarifa za kuaminika ni kuwa Agency inayomsimamia POS inapush biashara itokee na Simba hawana tatizo kwenye hilo huku wakiwa na uhakika wa kuletewa nyota wapya kutoka kwa Agency hiyo

Baadhi ya maeneo ambayo wanatarajia maingizo mapya ni eneo la ushambuliaji na Kiungo endapo Sakho ataondoka, hiyo ndio biashara ambayo huenda ikatokea kama POS ataondoka

Mpaka sasa Simba wamekamilisha saini moja tu ya kimataifa ambayo nina uhakika nayo, kama nilivyoripoti tangu mwezi Januari

Sakho ni moja kati ya wachezaji wenye usimamizi mzuri sana huku mitandao yake ya Kijamii inaendeshwa na Kaka yake aliyeopo nchini Senegal


Baadhi ya taarifa muhimu kuhusu dili hili nimepata kutoka kwa Mwandishi wa Senegal anayeishi nchini Ufaransa, ambaye ana ukaribu na wachezaji wengi wa Senegal
 
BAKARI MWAMNYETO TRANSFER UPDATE


Ni kweli kuwa Kitasa Bakari Mwamnyeto anaelekea mwisho wa mkataba wake pale Yanga Afrika, mwishoni mwa msimu huu

Yanga bado wanahitaji huduma ya nyota huyo na tayari walishafanya mazungumzo na Wakala wake Kassa Mussa (ambaye pia ni Shemeji yake) anaeishi nchini Italia

Wakala wa Bakari atawasili nchini mnamo mwezi wa tano kwa ajili ya mazungumzo na klabu ya Yanga kuhusu mkataba mpya wa Bakari Nondo na ofa zilizopo mezani

Klabu ambazo tayari zimeulizia huduma ya Bakari Nondo ni za nchini Misri, ambazo ziliamua kusubiri mpaka amalize mkataba wake kuepusha gharama kubwa za usajili

Kipingamizi kikubwa ni ‘offer matching’ ikiaminika upande wa Bakari utatazama kile ambacho Yanga wataleta mezani na kile ambacho klabu za Misri zitaleta mezani, ndipo maamuzi yatafanyika

Taarifa za uhakika kabisa ni kuwa SIMBA hawajatuma ofa yoyote kwa Wakala wa Bakari Nondo kuhusu kuinasa saini yake wala Simba hawajaonesha interests zozote kwa siku za hivi karibuni

Kama kuna uwezekano wa Simba kuanza mchakato basi ni mwishoni mwa msimu ila mpaka sasa hakuna mpango wowote

Hali ilivyo mpaka sasa kuna uwezekano mkubwa wa Bakari kuongeza kandarasi makutano ya Twiga na Jangwani, anatazamwa kama Mchezaji muhimu kikosini na Project ipo pembeni mwake
 
Hata ungekuwa mzee au kijana..
Kikubwa Upendo Uncle..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…