Makapuku Forum

Makapuku Forum

Elanga aliwahi kufuatwa na shirikisho la soka la Cameroon (FECAFOOT) ili kumshawishi avae jezi ya Simba asiyefugika

Elanga aligoma na akachagua kuendelea na timu ya taifa ya Sweden, bahati mbaya kwake ni kuwa Cameroon ipo kombe la dunia na Sweden wamefeli
Screenshot_20220403-195303_Instagram.jpg
 
• Watu watatu (wote Wanaume) wamefariki dunia na Mwanaume mmoja amejeruhiwa baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakiwa kwenye shughuli za machimbo ya mawe katika eneo la machimbo ya Kikikaka, Mji Mwema Kigamboni, Dar es salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa amethibitisha taarifa hizi na kusema miili mitatu ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Vijibweni na majeruhi amepatiwa matibabu na kuruhusiwa "Waliofariki ni Ally Fundi (18), Mohamedi Maganga (26) na Kashinde Msigale"

Nyangasa amesema "Machimbo haya yalishafungwa tangu mwaka 2018 lakini Watu walikuwa wanakuja kuchimba kwa kuibiaibia tu, niwakumbushe tena Wananchi bado maeneo haya yamefungwa hayaruhusiwi kuchimba na tutaweka ulinzi ili kuzuia Watu wasije"

"Wananchi wa eneo hili atakayekuwa na taarifa ya kutomuona Ndugu yake anayefanya shughuli zake hapa atuambie tuendelee na shughuli za ufuatiliaji, sio kwamba tumemaliza leo tutaendelea kufuatilia"
Screenshot_20220403-195652_Instagram.jpg
 
Mtanzania Felix Simbu amefanikiwa kuibuka mshindi wa tatu wa mbio za riadha (Milan Marathon zilizofanyika leo jijini Milan nchini Italia, huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Mkenya Kipruto Titus na nafasi ya pili ni Mkenya tena Kibet Kipkore.
Screenshot_20220403-200448_Instagram.jpg
 
Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika ya Kusini na Visiwa vya Caribbean, Vicky Ford amewasili Nchini kwa ziara ya siku tatu na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aliyeambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajabu.
Screenshot_20220403-200610_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom