Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewajeruhi kwa risasi Watuhumiwa watatu wa ujambazi (Mrisho maarufu Bonge na wenzake wawili) baada ya Watuhumiwa hao kupanga njama za kufanya tukio la ujambazi January 26,2022 saa mbili usiku Mbagala Zakhem karibu na duka la Rosemary Kimario ambaye ni Wakala wa Huduma za Kifedha (Tigopesa, Airtel Money, M Pesa, NMB, DTB na CRDB )
"Watuhumiwa hao wa Ujambazi wakiwa na pikipiki walifika eneo la tukio kwenye harakati za mwisho za kutaka kuvamia na kupora pesa lakini walibaini wanafuatiliwa na Askari Polisi walifika haraka eneo hilo ndipo Majambazi hao walianza kurusha risasi ovyo, Polisi walijihami na wakawashambulia Wahalifu hao ambao walijeruhiwa na kupelekwa haraka Hospitali lakini ilibainika wamepoteza maisha"
"Watuhumiwa hao walikutwa na Bastola ikiwa na magazine moja yenye risasi 11, pia walikutwa na noti bandia za elfu kumi zenye thamani ya Tsh. 1,180,000 ambazo hutumika kuwazubaisha Mawakala kama Wateja wanaotaka huduma kisha baadaye huwapora pesa halisi kwa kuwatishia kwa Bastola"
"Tunawataka Raia Wema kuendelea kutoa taarifa za Wahalifu mapema ili Jeshi la Polisi lifanye kazi ya kuzuia matukio hayo" Muliro Jumanne Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam