Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220121-081524_Opera%20Mini.jpg
 
Polisi mijini Free Town nchini Siera Leone wamekesha kulinda nyuma ya mshambuliaji wa timu ya Taifa ya nchi hiyo Kei Kamara aliekosa penati kwenye mchezo dhidi ya Equatorial Guinea.

Mashabiki hao walitaka kuichoma moto nyumba hiyo kwasababu tu mchezaji huyo alikosa penati na kusababisha timu yao ya Taifa kutolewa kwenye michuano ya AFCON huko nchini Cameroon.
Screenshot_20220121-103320_Instagram%20Lite.jpg
 
CONFIRMED: POLISI, YANGA KUPIGWA ARUSHA
.
Uongozi wa timu ya soka ya Polisi Tanzania umethibitisha kupeleka mchezo wao dhidi ya Yanga katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
.
Mchezo huo ulipangwa kupigwa Jumapili katika uwanja wao wa Ushirika lakini siku moja kabla ya mchezo yani Jumamosi kutakuwa na tamasha la Utamaduni Mkoa wa Kilimanjaro ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hivyo imeilazimu uongozi wa timu hiyo kuhamishia mechi hiyo Arusha.
.
Inaweza kuwa ni habari njema kwa Yanga kwani wenyewe tayari wameweka kambi Arusha kujiandaa na mchezo huo.
Screenshot_20220121-103646_Instagram.jpg
 
HATUA YA 16 BORA AFCON
.
Morocco Malawi
Cote d’Ivoire Egypt
Senegal Cape Verde
Nigeria Tunisia
Mali Equatorial Guinea
Burkina Faso Gabon
Cameroon Comoro
Guinea Gambia

.
Nani kubeba ndoo ya AFCON 2021 __!!

Screenshot_20220121-103850_Instagram.jpg
 
BARCELONA HAS FALLEN

- Katolewa kwenye UEFA ameenda EUROPA

- Kapigwa SUPERCUP na Real Madrid

- Jana kapigwa tena na Athletic Club, Katolewa 16 Bora kwenye Kombe la Mfalme

Barcelona
Screenshot_20220121-104037_Instagram.jpg
 
Opah Clement Sanga bila shaka ndie Mchezaji Bora zaidi kwenye Ligi ya Wanawake mpaka hivi sasa

Analijua goli, anaujua mpira na ni Mchezeshaji mzuri sana, inavutia sana kuitazama Simba Queens

Kule mbele awepo OCS + Asha Djafar
Screenshot_20220121-104200_Instagram.jpg
 
KIBU, MKUDE KUIKOSA MTIBWA:

Wachezaji wa Simba, Jonas Mkude na Kibu Denis hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kitakachosafiri kuelekea Morogoro kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Siku ya Jumamosi kufuatia kuwa majeruhi.

Wachezaji hao walipata majeraha katika mechi dhidi ya Mbeya City ambapo walishindwa kuendelea na mchezo kipindi cha pili.

Taarifa ya Klabu ya Simba imeeleza kuwa, nyota hao wanaendelea vizuri na wamepumzishwa iii hali zao zirejee katika utimamu na wanatarajia kuwepo katika michezo itakayofuata.
Screenshot_20220121-104851_Instagram.jpg
 
PIGO: Mwakinyo, Ibra Class Wavuliwa Mikanda
.
Habari mbaya kwa mabondia bora nchini, Hassan Mwakinyo na Ibrahim Class ni kuvuliwa kwa mataji ya ubingwa wa WBF.
.
Mabondia hao wamevuliwa mikanda hiyo ya ubingwa na Shirikisho la ngumi za kulipwa la dunia la WBF. Taarifa iliyotolewa na WBF imeeleza kuwa mabondia hao si mabingwa tena wa mikanda ya WBF kwenye uzani wa super welter na super feather ambayo walikuwa wakiishikilia Mwakinyo na Class hivyo iko wazi.
.
“WBF tumeumizwa na hiki kilichotokea, lakini kwa mujibu wa kanuni, hawa si mabingwa wetu tena baada ya kushindwa kutetea ubingwa kwao kwa wakati,”
Screenshot_20220121-114340_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom