Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220118-054916_Opera%20Mini.jpg
 
PABLO ATIA NENO KIWANGO CHA BOCCO
.
“Inatokea tu mchezaji kuna wakati inakuwa hivyo, sio kusema Bocco hajui hapana, ni namna ya mchezo unavyokuwa na ushindani wake,
.
“Unakuta pia mchezaji anajipanga kweli kweli kuhakikisha anafanya kile anachokitarajia akini ikitokea akakwama, inamuumiza hata yeye mwenyewe,” amesema Pablo na kuongeza:
.
“Bocco ni mchezaji mzuri na ndio maana ni nahodha na mimi nafahamu namna ambavyo anajisikia kutokana na msimu uliopita alivyofanya vizuri lakini kwa sasa hajafanya vile,”
.
WANASIMBA mmemsikia Pablo anasema ni suala la muda Bocco gari litawaka __!!
Screenshot_20220118-073514_Instagram.jpg
 
WAKALA AGUSIA YANGA NA SIMBA DILI LA MSUVA
.
Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kufanya mazungumzo na winga Simon Msuva, lakini alishikilia msimamo wake wa kutaka kuendelea kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.
.
Yanga walikuwa tayari kumpa mkataba wa miezi sita mchezaji huyo ili mara baada ya msimu kumalizika aendelee na harakati zake za kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania jambo ambalo liligonga mwamba.
.
Baada ya dili hilo kukwama, Simba nao walimfuata na kuhoji uwezekano wa kupata huduma yake, hali ikawa kama ilivyokuwa kwa Yanga ambao walikuwa tayari kutoa zaidi ya milioni 100.
.
Fikra na mawazo ya Msuva kwa sasa ni kuendelea kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania ndio maana ilikuwa rahisi kwake kugomea ofa za klabu hizo.
Screenshot_20220118-093810_Instagram.jpg
 
Zlatan Ibrahimovic:

"Ninaumia sana ninapokosa nafasi ya wazi ya kufunga bao, sio kukosa Penati. Ninapofunga Penati nahisi kama nimefunga tu kwenye mazoezi sioni haja ya kupiga kelele kushangilia na kurukaruka kwa ajili ya bao la Penati.

Shangilia ya kweli inakuja pale ninapofunga kwenye mchezo wa wazi wakati kila mtu ananikaba, basi najua bao hilo linaweza kurekodiwa kwa kujivunia katika vitabu vyangu, sio Penati ambapo kila mtu anasimama nyuma yangu na kuniacha tu nikikabiliana na Kipa asiye na msada wowote.”
.
Hapa mnakubaliana na Zlatan eti mabao ya penati sio ya kushangilia __!!


Nampendaga Zlatan mswahili mwenzangu
Screenshot_20220118-184954_Instagram.jpg
 
MKUDE ATIA NENO MORRISON KUDAI ANAMFUNDISHA MATUSI
.
Hivi karibuni staa wa Simba, Bernard Morrison aliweka wazi kuwa Mkude ndiye mtu anayemfundisha Lugha ya Kiswahili na amekuwa akimfundisha pia kuzungumza matusi.
.
"Hahaaa, hivi unadhani mimi naweza kumfundisha matusi yule mtu mzima. (Anacheka tena) mimi siwezi 'bwana' yule ni mtu mzima sana kwangu.”
.
"Nampenda sana maana yeye ni rafiki yangu tunayeshirikiana kwa mambo mengi sana ndani na nje ya uwanja."
Screenshot_20220119-141734_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom