Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220119-142031_Instagram.jpg
 
Ukiachana na matokeo ndani ya uwanja, kuna vitu vingi sana vya kujifunza kutoka kwenye michuano ya AFCON 2021 inayoendelea Cameroon.

Exposure kwa wachezaji imekuwa kubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma, maendeleo ya temnolojia yamerahusisha upatikanaji wa maudhui ya mpira.

Zamani ilikuwa kimbembe kufatilia mechi zote za AFCON pamoja na Ligi nyingine za Ulaya lakini kwa sasa mambo ni tofauti.

Ukirudi ndani ya uwanja unakuta mambo yapo tofauti tena! Ghana anakula za uso na nchi ambayo huenda miaka kadhaa nyuma walikuwa wanaaiangalia ikishindana na nchi nyingine kwenye mashindano haya.

Comoros wananufaika na uraia pacha, wachezaji wao wengi hawajazaliwa Comoros lakini baada ya FIFA kuruhusu mchezaji ambaye amezaliwa taifa jingine kuitumikia timu ya taifa ambayo ya nchi ambayo ana vinasaba nayo imewafanya Comoros kuwa na timu bora.

Wachezaji wengi wa Comoros wanacheza Ulaya japo sio kwenye timu zinazocheza madaraja makubwa lakini tayari wana misingi ya soka tangu utotoni.

Ghana ambao ni mabingwa mara nne wa taji la Mataifa ya Afrika jana walikuwa wanautaguta mpira!
Screenshot_20220119-144306_Instagram.jpg
 
Paul Pogba amewaambia Manchester United kuwa anahitaji kuondoka mwishoni mwa msimu huu huku wengi wakiamini anahitaji kujiunga na Real Madrid ya Hispania
Screenshot_20220119-145052_Instagram.jpg
 
Mario Balotelli NEWCASTLE UNITED
.
Newcastle United inataka kumsajili straika wa Adana Demirspor mtukutu wa Kiitaliano, Mario Balotelli, 31, katika dirisha hili ili kwenda kuongeza nguvu kwenye eneo lao la ushambuliaji linaloonekana kuwa na udhaifu kwa msimu huu. Mkataba wa sasa wa staa huyo unatarajiwa kumalizika mwaka 2024. Msimu huu amecheza mechi 20 za michuano yote na kufunga mabao nane.

Screenshot_20220120-115650_Instagram.jpg
 
SUAREZ NAYE KUTUA ASTON VILLA SI BALAA HILO
.
Steven Gerrard mpango wake sio poa kabisa kwa wapinzani. Anachotaka ni kuwarudisha Aston Villa kwenye michuano ya Ulaya. Hivi karibuni, chama lake hilo lilinasa huduma ya kiungo fundi wa mpira, Philippe Coutinho, ambaye waliwahi kucheza pamoja Liverpool. Na sasa kinachoelezwa, mchezaji mwenzake mwingine wa zamani huko Anfield, Luis Suarez, naye anataka kwenda kukipiga Villa Park. Si itakuwa balaa hilo.
.
Kwa mujibu wa taarifa kutok Hispania, Suarez ameweka wazi mpango wake wa kwenda kujiunga na Aston Villa. Mkataba wa staa huyo mwenye umri wa miaka 34 huko Atletico Madrid utafika tamati mwisho wa msimu huu na inaelezwa amezigomea ofa za timu kibao ili akamilishe ndoto za kwenda kucheza chini ya swahiba wake wa zamani, Gerrard.
Screenshot_20220120-115811_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

USIKU WA ABUNUASI NA NDOTO ZAKE

Ilikuwaje alipoamka ule usiku wa manane baada ya ndoto ndefu ya kutisha? Najua alipoamka mlimpa maji na kumwambia ajikaze awasimulie

Anasema mwisho wa gili yetu aliona Braza wetu wa jeans kuchanika akishangilia, aliona 'wakazi' wakifurahi kwa nderemo na vifijo, ama kweli mwaka wao huu

Anasema ndotoni aliwaona wakiripoti kwenye chiko lenye rangi ya theluji, mwanzo walifika kusalimia, baadae wakaja kuleta shida zao

Siku ya tatu wakasaidiwa shida na siku ya nne walipaswa na wao kusaidia kutatua shida! Kwani Mwalimu historia si alisema There's no free lunch in capitalist system

Anasema ndotoni alimuona Dada mmoja mrembo sana tena na niwami yake usoni, wengine wanasema Dada kamind kuhusu ile clip ya leyema Wachezaji wakishangilia inaonekana wameipenda, we si ndio unapenda Uafrika na kuutukuza Uzungu

Lakini shida nini? Watu wamesahau the game is fair play?? Tena kwenye ndoto anasema hata wale Wazee wa habari kiganjani huenda wakala pin wasifike mazoezini, ni hatari lakini salama, bwana we ndio hatari ya degree za 'Michuu' kuongoza mpira

Nasikia aliota kwa muda mrefu, kipi kingine tena? Nasikia yule Mnyama BIG FIVE mbugani anaitaka ndoo ya tano tena! Lakini katika hali ya kawaida, kibinadamu na kiungwana wetu wa 'Kiafrika' nadhani haiwezekani

Shida nini kwani? Hakuna shida ila ni ngumu chapati kuchomwa tu upande mmoja, ndoto inasema raha ya chapati ichomwe pande zote, Ili tupate KURA hapana sorry, namaanisha KULA

Kwahiyo?? Nasikia mzigo tayari umewekwa! Kwani ndoto inasemaje?? Ndoto inasema Kuna akaunti maalum, ile faida ndio inaenda kwa Mnyama BIG FIVE, lakini sina uhakika maana ni ndoto tu

Kumbuka wewe Mtoto Bado Mdogo ujue?? Basi tu naomba ufahamu Wangindo sisi tunasema "Ndumba ya mtoto Mkubwa anakula, Ndumba ya Mkubwa na Mtoto anakula"
Screenshot_20220120-115945_Instagram.jpg
 
"Ratiba yetu inatubana sana, tumecheza tangu mwezi Novemba 2021 bila kupumzika, wachezaji wangu wamechoka na hata mechi ya Jumapili nimeamua kuwapa mapumziko ya siku mbili na tutafanya mazoezi siku mbili tu kabla ya kukutana na Tottenham" Thomas Tuchel, Kocha wa Chelsea
Screenshot_20220120-120432_Instagram.jpg
 
Kampuni ya kutengeneza vyombo vya moto vinavyotumia umeme nchini Kenya inayoitwa Opibus imetangaza kujiandaa kuingiza sokoni Mabasi ya Umeme yanayotengenezwa nchini Kenya, Kampuni hiyo inasema hayo yatakuwa Mabasi ya kwanza ya umeme kutumika Afrika.

Kampuni hiyo inayomilikiwa na Wakenya kwa ushirikiano na Watu wa Sweden imesema itaanza na Mabasi 10 ya majaribio ambayo yataingia sokoni katikati ya mwaka huu 2022 na yatauzwa kwa gharama ya hadi Ksh Milioni 11.3 (Tsh. Mil
223.738 ) .

Malengo ya Kampuni hiyo ni kuwa na Mabasi ya Umeme mengi ambayo yatasaidia kupunguza foleni katika Jiji la Nairobi huku yakiwaingizia Wamiliki fedha, Mabasi hayo yatakuwa yanachajiwa na kuwa full ndani ya saa moja.

Mwezi December mwaka jana Kampuni hiyo ya Opibus ilitangaza pia kushirikiana na Kampuni ya Uber na kusema wataingiza sokoni Pikipiki za Umeme 3000 ambazo zitarahisisha shughuli za usafiri Kenya.
Screenshot_20220120-150252_Instagram.jpg
 
Kituo kimoja cha kutolea huduma za matibabu kilichopo Mombasa Kenya kimetakiwa na Mahakama kulipa fidia ya Ksh. milioni 2 (Tsh. milioni 40) kwa Mgonjwa aitwaye Roberto Macri baada ya kumpa majibu ya uongo ya vipimo kuwa ana cancer wakati hana cancer.

Jaji wa Mahakama ya Malindi, Julie Oseku amesema Mgonjwa huyo alifika Kituoni hapo 'Jamu Imaging Centre' akiwa na changamoto ya kupata shida ya kumeza chakula na akaambiwa ana 'Cancer Stage Four' hali iliyomlazimu kusafiri hadi Italia ambako aliambiwa hana Cancer.

"Mgonjwa kama asingeambiwa ana Cancer asingelazimika kutumia gharama kwenda Italia baada ya kuwa na hofu, pia majibu yalimsababishia stress na maumivu zaidi ndio maana aliporudi tu kutoka Italia akafungua kesi" ——— Mahakama.
Screenshot_20220120-150405_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom