MUKOKO AFUNGUA KISA CHA KUIGOMEA YANGA
.
Dili la Kiungo na nahodha msaidizi wa Yanga, Mukoko Tonombe kwenda TP Mazembe ya DR Congo, limekufa baada ya nyota huyo kugoma kutolewa kwa mkopo katika klabu hiyo, huku bilionea wa klabu hiyo Ghalib Mohamed ‘GSM’ akiingilia kati.
.
Mukoko amesema mbali ya kufanyiwa taratibu zote ikiwemo kukatiwa tiketi ya kwenda Lubumbashi alishindwa kusafiri kutokana na kushindwa kufahamu hatma yake kwamba anaenda TP Mazembe kama mchezaji wa mkopo au anauzwa moja kwa moja na kumfanya aende moja kwa moja kumuona Bilionea wa GSM.
.
“Bosi ameniambia nisiende kokote nitabaki hapa Yanga mpaka mwisho wa msimu utakapomalizika na baada ya hapo ndio kutakuwa na mazungumzo mengine kati yetu,” alisema Mukoko na kuongeza;
.
“Nimeambiwa keshokutwa nitapewa tiketi ya ndege kwenda kujiunga na timu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania.”