

Farhan Jr
HANCE MASOUD NA UTATA WA USAJILI

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye vyanzo vyangu ni kuwa Hance Masoud ambaye ni beki wa zamani wa Coastal Union yupo kwenye utata mkubwa wa usajili

Hance alisaini mkataba wa awali na klabu ya Dodoma Jiji wakati akielekea mwisho wa mkataba wake na Coastal Union, huku akipokea sehemu ya fedha za usajili huo

Lakini baadae kulitokea na sintofahamu juu ya Hance kuripoti Dodoma, Kutokana na pia na sababu mbalimbali, ikasemekana atabaki Coast na watampa mkataba mpya

Kutokana na kuwa Dodoma hawakuhitaji kuharibu mahusiano yao na Coast walikubali na wakaomba kiasi chao cha fedha kwa Mchezaji Ili wamuache huru na waendelee na taratibu zingine

Lakini wakati Dodoma wameomba fedha yao, Hance pia alishindwana na Coast kwa issue ya maslahi hivyo isingewezekana kwa Hance kusaini tena Coast

Katikati ya issue hii, wakati Dodoma wanasubiri mzigo wao, wakapokea simu kutoka kwa Viongozi wa Coast kuwa wanaweza kuendelea na utaratibu wao wa kumsaini Kijana, Hivyo Dodoma kwakuwa tayari wana precontract wakatuma details zote TFF

Na mfumo wa TMS umempitisha Hance kuwa ni Mchezaji Halali wa DODOMA JIJI huku taratibu za leseni zikiendelea hivi sasa

Wakati haya yote yakiendelea, KMC na Hance Masoud wamefikia makubaliano ya kusaini mkataba, ila kwenye system anasoma kuwa ni Mchezaji wa Dodoma, hawawezi kufanya kitu bila kumalizana na DODOMA JIJI

Wakati huo Mchezaji anadai yeye ni Free Agent, Dodoma wanasema kama yupo free basi waendelee na taratibu zingine! Dirisha pia linaelekea mwisho usiku wa leo