Mahakama kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi imetupilia mbali mapingamizi mawili yaliyotolewa na upande wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu na kupokea hati ya ukamataji mali.
Mbowe na wenzake hao, Halfan Bwire, Adamu Kasekwa na Mohamed Ling’wenya wanakabiliwa na kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Joachim Tiganga.
Uamuzi huo unahusu mapingamizi mawili ya mawakili wa utetezi katika kesi hiyo ambayo ni orodha ya vielelezo na mnyororo wa utunzaji vielelezo.
Akitoa uamuzi huo leo Ijumaa Desemba 17, 2021 Jaji Tiganga amesema mahakama inapokea kielelezo hicho na kinakuwa ni kidhibiti cha 14.