

Farhan Jr
SIMU YA PROFESA, SIMBA VS GEITA
Kwanza kabisa lile ni goli la wazi kabisa ambalo Geita wamenyimwa na LINE 1, sio kosa la Mwamuzi wa kati bali LINE 1
Baada ya mpira kuwekwa tu kimiani, Mwamuzi wa kati aligeuka kuonesha Kati kabla ya LINE 1 Kigoma kuwa ni faulo, ila Mwamuzi wa kati alipitisha kuwa ni goli ila shida ya Msaidizi wake
Turning point ya mchezo wa leo ni baada ya kumtoa Rally Bwalya, hauwezi kuwa na timu ya Mzamiru, Mkude, Kibu wote ndani bila kuwa na Mpishi mmoja ambaye ni Bwalya
Ikawa ni rahisi sana kwa Geita kuwazidi Simba eneo la Kati, ndipo hapo Yusuph Kagoma na Nashon Naftali walipopata nafasi ya kucheza mpira wao kirahisi sana
Nimemtazama vyema sana John Bocco, changamoto yake leo ni ya kimfumo Wala sio kwamba ameisha hivyo! Simba inacheza zaidi kutokea pembeni na setpieces
Nilikuwepo uwanjani, nikawa namtazama Bocco wakati timu inafanya transition, mara nyingi alijikuta off position ama mpira anapewa kwenye Watu! Bocco sio holder mzuri wa mpira, anahitaji kusimama huduma zije
Defense ya Simba leo ilivuja sana na ndio ilikuwa inakaribisha mashambulizi, shukrani kwa mikono ya Aishi Manula! Shida ya kwanza ni mstari Kati ya Banda na Gadiel, Kulikuwa na gap kubwa sana
Shida nyingine ni beki ya Kati! Onyango na Juma wazuri sana ila wanamkosa Kiongozi mmoja, kuna muda walikuwa wanafuatana sana na kufanya uwanja uwe mkubwa sana
Hata pale waliposhambuliwa sana walistick bado kwenye pass fupi ama kubutua, ile akili ya Pascal Wawa inahitajika mapema, uwezo wa pass na kusoma Mchezo ila tu juu yake awepo Onyango au Juma
Peter Banda ni exceptional talent kama nisemavyo siku zote ijapo mlinitukana sana ila muda utaongea