[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
Captain Hlompho Kekana wa Mamelodi Sundowns alijumuishwa kwenye kikosi cha AFCON 2019 cha Bafana Bafana ila bahati mbaya hakuwa akianza kwenye kikosi
Swali la kwanza la Wanahabari ni kuwa mbona muda wote alikuwa mtiifu sana mazoezini na alikuwa anahamasisha sana wenzake? Licha ya kwamba hapati nafasi kikosini
Kekana aliwajibu kuwa kuna Kekana wawili ndani ya nafsi moja! Kuna Kekana Mcheza mpira na kuna Kekana Raia wa Afrika Kusini ambaye ni Shabiki mkubwa wa taifa lake
Captain Fantastic alimaliza maneno yake ni ilikuwa rahisi kumuelewa, kama hatoanza kama Mchezaji basi atakaa kwenye bench na kuwashangilia na kuhamasisha wenzake kwa kofia ya Uzalendo na Ushabiki kwa Taifa lake
Well leo nilitulia kwenye mechi nzuri sana kati ya Taifa Stars dhidi ya Benin! Awali ya yote nilivutiwa sana na picha iliyopostiwa na kurasa rasmi za @tanfootball , macho yangu yalinasa kwa Idi Seleman Nado
Alisimama mbele zaidi kapiga goti na umakini mkubwa akimsikiliza Kocha Kim Poulsen, ni ngumu kuamini kuwa Iddi mwenyewe anajua haanzi au hatopata nafasi ila nafsi na roho yake zipo tayari kwa ajili ya taifa lake
Ananikumbusha pia alipoulizwa David Silva kwanini alikuwa makini sana kumsikiliza Kocha Del Bosque, nae akasema ni bahati kufundishwa na Kocha kama huyo pale Hispania, kama hatoanza mbele ya wakina Iniesta na Xavi basi anapata elimu ya kwenda nayo Valencia
Tukio la pili la Iddi Seleman Nado ni pale Stars inashambuliwa, nilikuwa nastream live kupitia FIFA TV! Licha ya kuwa hachezi ila sasa yeye ndie Shabiki mkubwa wa Taifa lake wakiwa ugenini, hajasomea Ukocha ila alisimama kutoa maelekezo peke yake
Alisimama kuwakumbusha wenzake, licha ya kuwa hachezi ila walau maneno yake yatawasaidia kwenye mapambano kule Benin, bila kinyongo kwakuwa anafanya kwa ajili ya taifa lake
Nilipenda passion yake nilipenda mahaba yake kwa taifa lake hongera sana nado