Makapuku Forum

Makapuku Forum

IMEVUJA| Orodha ya wachezaji 30 kwenye kinyang’anyiro cha Ballon dor mwaka huu
Screenshot_20211008-195038_Instagram.jpg
 
Mechi [emoji2391]
Ushindi [emoji2391]
Alama [emoji2397]

Mikel Arteta wa Arsenal ndie Kocha bora EPL mwezi Septemba

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Screenshot_20211008-195234_Instagram.jpg
 
Kwangu kucheza timu ya Taifa ilikuwa ni kila kitu, bahati nzuri nilianza kucheza tangu timu za Taifa za vijana kwa hiyo nilianza kuwa na hamu ya kuwa mchezaji wa timu ya Taifa. Na huko unakoanzia hakuna kitu zaidi ya ile fahari tu ya kucheza timu ya Taifa.

Kwa mchezaji kupigiwa wimbo wa Taifa ni kitu ambacho huwezi kukutananacho kama haupo timu ya Taifa. Wakati mwingine kuna vitu navipa thamani kuliko hata pesa, ndio vilikuwa vinanipa chagizo ya kufurahi au kusikitika ninapokuwa nje ya timu ya Taifa.

Zamani vilabu vinavyoshiriki mashindano ya kimataifa vilikuwa vinapigiwa nyimbo za Taifa lakini waliondoa kwa sababu kuna nyakati unakuta karibu wachezaji wote wageni halafu wanapigiwa wimbo wa Taifa.

- Amri Kiemba, Mchezaji wa zamani Taifa Stars
Screenshot_20211008-195519_Instagram.jpg
 
'Chaboli' Jack Wilshere akiwa mazoezini London Colney ambavyo ni viwanja vya mazoezi vya Arsenal

Arsenal wamemruhusu Kijana wao atumie miundombinu yao kipindi hiki anajiweka sawa na akiendelea kusomea Ukocha

Mtoto karejea nyumbani na jezi wamempa za mazoezi FOOTBALL[emoji119]

Wakati huku kwetu Magwiji hata tiketi ya uwanjani hawapewi
Screenshot_20211008-195817_Instagram.jpg
 
The Magpies hao Newcastle United ina wamiliki matajiri zaidi duniani wakiwapiku PSG ambao walikuwa wanaongoza

Newcastle - £320 Billion
PSG -£220 Billion

Arab [emoji383]
Screenshot_20211008-200122_Instagram.jpg
 
"Kiungo wa Taifa Stars, Mzamiru Yassin atakosa mechi ya Jumapili dhidi ya Benin kutokana na kuwa na kadi mbili za jano. Pengo lake litazibwa na Zawadi Mauya.
.
“Mzamiru ana sifa moja kubwa nayo ni kujituma. Huyu ni punda wa timu...haoni tabu kupigwa chenga, kuingiza mguu sehemu ngumu...ni mzuri zaidi kwenye interception. Ni pengo kwa Taifa Stars.

- Michael Mwebe.
Screenshot_20211008-200403_Instagram.jpg
 
Hatma ya Pogba Man United Kizungumkuti !!
.
Kiungo wa Manchester United na Ufaransa, Paul Pogba amefunguka juu ya hatma yake na uwezekano wa kurudi Juventus
.
“Ninapapenda Torino! huwa nazungumza na marafiki zangu wa zamani wanaocheza Juve kama Dybala. Kwa sasa nipo Manchester, niko chini ya mkataba hadi Juni 2022 baada ya hapo tutaona nini kitatokea. Nataka kumaliza msimu huu kwa kiwango bora - ndipo tunaona ”.
.
Ikumbukwe kuwa United tangu Julai inambembeleza Pogba kuongeza mkataba wenye mshahara mnono lakini mwamba Paul Labile bado hajakubali kusaini.
Screenshot_20211008-200528_Instagram.jpg
 
Serikali ya Uingereza imetangaza rasmi kuiondoa Tanzania katika orodha ya Nchi ilizoziwekea vikwazo vya usafiri kutokana na janga la Covid 19 na sasa kuanzia October 10, 2021 Msafiri kutoka Tanzania hatokaa karantini akiingia Uingereza lakini sharti awe amepata moja ya chanjo nne ambazo Uingereza inazitambua ambazo ni Pfizer-BioNTech, Oxford- AstraZeneca, Moderna na Janssen na kwa zinazohitaji kuchomwa mara mbili Mtanzania atatakiwa awe amechoma mara zote mbili.

Tanzania sasa inaingia kwenye orodha ya Nchi nyingine 47 ambazo zimeondolewa kwenye red list ‘list nyekundu’ ya Uingereza ambapo sasa ni Nchi 7 pekee zimebaki kwenye red list ya kutoingia Uingereza ambazo ni Peru, Ecuador, Colombia, Panama, Haiti, Venezuela na Dominican Republic.

View attachment 1968492
Hii ni habari nzuri sana kwa wafanyabiashara na wasafiri wanaotegemea kufika UK
 
Back
Top Bottom