[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
ALI KIBA, DARASA LINGINE LA MZIKI LITAISHI MILELE
Kwenye soko la mziki duniani kuna vitu viwili vinaamua aina ipi ya mziki ufanyike! Kuna Trend per Music na Music per trend! Hivi hupelekea muda mwingine kupoteza maana ya muziki
MUSIC PER TREND! Ni kupelekwa na upepo wa aina gani inasumbua sokoni! Mfano Afrika hivi sasa Amapiano imekamata sana, lakini huu ni mziki wa Afrika Kusini, huwezi kufanya zaidi yao na ukiufanya ni kuuza zaidi flavour yao
Wasanii wengi Tanzania wametoa ngoma za Amapiano, lakini hizi ngoma haziishi sana, ngoma hizi pia zinapoteza utambulisho wa mziki wa Tanzania kwenye soko la Afrika, haswa kipindi hiki watu wanapambana mziki wetu utoboe
Wakati Wasanii wengi wakubwa wamekubali kuishi utamaduni wa Wasauzi kwenye nchi huru Tanzania, ni Ali Kiba anakuja kutupa album yake yenye mziki wake bila Amapiano hata moja! Hakuna hata wimbo mmoja ulisukumwa na upepo wa sasa
Huyu ndie Ali Kiba ninaemfahamu, anaishi kwenye ile misingi yake, ndio maana ngoma zake zinaishi sana kwakuwa hazina mlengo wa upepo, unaweza kusikiliza kuanzia Mapenzi Yanarun dunia hadi Oya Oya! Bado ukamuona Kiba ni yule yule
Anaendelea kuulinda mziki wa Tanzania dhidi ya upepo mkali wa Wasauzi, wanaopambana kuupenyeza mziki wao Afrika! Tujiulize SINGELI ni mziki wetu ila umepata mileage kubwa nje? Jibu ni HAPANA, lakini wenzetu wametuteka
Kingine ni TREND PER MUSIC! Ni darasa lingine Kiba anaendelea kuwapa vijana chipukizi wanaotaka kufanikiwa zaidi, tuulizane KIBA ametoa album yake umeona kuna Kiki kazifanya? Umeona kuna skendo kazifanya?
Kiba mziki wake unaishi sana kwakuwa anaandika kutaka uishi na atawale mioyo ya watu, ukifanya kiki utaandika ili utawale vichwa vya watu, kumbuka kichwa kina mengi kinasahau, ila moyo hausahau kamwe