Makapuku Forum

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakipo tayari kukutanishwa na jeshi la polisi, kama ambavyo ametangaza Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ili kuondoa mvutano kati yao, vyama vya siasa na jeshi hilo.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Septemba, 7,2021 na Mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alipozungumza na waandishi wa habari.

Mrema amesema hawaoni haja ya kukutanishwa na jeshi hilo kwa kuwa kwa mambo ambayo wamekuwa wakiyafanya kwa miaka sita amedai ni wahalifu ambao wangetakiwa wawe wameshafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
Mradi wa mabasi ya mwendokasi mkoani Dar es Salaam, umeongeza ruti za safari za mabasi hayo na sasa umeanza kutoa huduma zake hadi Kawe.

Hii inakuja ikiwa ni siku chache tangu kuongezwe ruti ya Morocco- Mwenge iliyoanza Agosti 27, 2021 na hivyo kuwafanya wakazi wa Mwenge kuwa na ruti mbili za mabasi hayo, ukiacha ile ya Shekilango-Mwenge iliyoanza Agosti 26, 2021.

Katika ruti zote hizo nauli ni Sh400 huku ile ya Kawe ikiwa imeanza Septemba 2, 2021.

Msemaji wa wakala huo, Willium Gatambi amesema ni katika kuendelea kutoa huduma katika njia za mlisho ambazo vituo vyake vilijengwa muda mrefu.

Amesema vituo hivyo viliwekwa mahususi kwa ajili ya watu wanaotoka pembezoni mwa mji, ambapo wakifika hapo wanaunganisha usafiri wa mabasi hayo katika njia kuu.
 
Idadi ya masomo katika mtihani wa darasa la saba mwaka huu imeongezeka kutoka masomo matano hadi sita, somo lililoongezeka linaitwa uraia na maadili. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dk Charles Msonde ameeleza
 
Kundi la Taliban limetangaza serikali ya mpito nchini Afghanistan ambayo itaongozwa na Mullah Mohammad Hassan Akhund, huku mwanzilishi mwenza wa kundi hilo, Mullah Abdul Baradar akiwa msaidizi wake.

Kundi hilo limewahi kuiongozo Afghanistan kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 2001.
 
El Salvador imekuwa nchi ya kwanza kukubali sarafu za kidijitali za Bitcoin kuwa fedha halali, uamuzi ambao umeibua mjadala duniani, kutokana safaru hiyo kupanda na kushuka thamani kwa haraka.

Mashine 200 zimewekwa kwenye maeneo mbalimbali nchi humo kubadili dola kuwa Bitcoin.
 
Mahakama nchini Vietnam imehukumu Le Van Tri kifungo cha miaka 5 gerezani kwa kosa la kusambaza virusi vya corona, baada ya kukiuka masharti yaliyowekwa. Tri amesambaza ugonjwa huo kwa watu nane, ambapo mmoja amefariki.

Taifa hilo limeripoti visa 530,000, vifo vikiwa ni 13,000.
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai ameeleza kushtushwa kupitishwa kwa sheria inayomtaka mkulima kulipa ushuru wa bidhaa wa asilimia mbili kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati Kamati ya Bunge ya Bajeti ilikataa.

Amesema kamati inapopinga jambo, lakini serikali ikaendelea kuling'ang'ania huwa ni majanga kwa wananchi. Aidha, amesema endapo kamati yoyote itakutana na hali kama hiyo tena, itoe taarifa bungeni ili bunge liwe upande wa kamati na waziri husika abaki mwenyewe.
 
JeWajua

Pasipoti ya Tanzania ni ya 77 kwa uimara dunia (ikifungana na Kenya na Indonesia) ambapo ukiwa nayo utaweza kuingia katika nchi 72 bila kuhitaji visa.

Pasipoti imara zaidi Afrika ni ya Shelisheli (28 dunia), mwenye nayo anaweza kuingia nchi 152 bila kuhitaji viza.
 
Wanafunzi wa kike na wa kiume wakiwa wametenganishwa kwa pazia darasani katika moja ya vyuo nchini Afghanistan ikiwa ni mabadiliko chini ya utawala wa Taliban.

Mara ya mwisho kundi hilo lilipoitawala nchi hiyo (1996-2001), lilizuia wanawake kwenda shule, vyuoni na kufanya kazi.
 
Dah anajifeel vipi ticha?
 


Sent using Jamii Forums mobile app
 
KANALI MAMADY DOUMBOUYA

.......Jana kanali Mamady doumbouya alipindua serikali ya Guinea conarky iliyokua chini ya Rais alpha Conde.

Rais Alpha Conde alibadilisha katiba mwaka 2020 na kugombea Urais kwa awamu ya tatu baada ya awamu zake mbili kikatiba kuisha..

Kanali Mamady Doumbouya ni nani.....????

Kanali Mamady Doumbouya ni mwanajeshi hatari aliyepata mafunzo ya juu katika upande wa kutambua na pia kupambana kwa haraka sana na hatari yoyote itakayojitokeza na kuirudisha hali ya nchi katika usalama wake wa kawaida....

Alikua ni mkuu wa Guinea special forces toka mwaka 2018 alipoitwa nchini humo toka ufaransa....Guinea Special force ni kikundi maalumu cha kijeshi ndani ya jeshi la Guinea chenye kazi ya kuzima jaribio lolote hatari kwa haraka sana litakalokua hatari kwa usalama wa Rais na nchi pia.

Ni mwanajeshi mwenye uzoefu wa miaka 15 ya operation za kijeshi duniani...alihusika katika operational hatari za kijeshi duniani kama

operation za kijeshi Afghanistan dhidi ya Talibani

Alikuwepo katika operation za kijeshi ivorycoast dhidi ya Waasi

Alikuwepo katika operational za kijeshi Djibouti na Afrika ya kati pia....

Amepata mafunzo yake ya kijeshi katika nchi za Islael,Ufaransa,Uingereza,Senegal,Cyprus na Guinea kwenyewe.

Ana masters degree katika Defence and industrial dynamic aliyoipata katika chuo kikuu cha Pantheon huko Paris.
 
πŸ’ͺ🏿πŸ’ͺ🏿πŸ’ͺ🏿πŸ’ͺ🏿πŸ’ͺ🏿
 
Hizi hawapati wateja sana... Kama huko mbezi na kimara (mbagala) ikishakamilika
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…