Makapuku Forum

UNAAMBIWA

Nchini Rwanda Jeshi la Polisi hutumia camera maalum zilizofungwa kwenye maeneo mbalimbali kufahamu mwendo wa magari barabarani ambapo gari linalokimbia kuliko spidi inayotakiwa hupigwa picha na camera hizo na kisha msg ya kulipa faini kutumwa kwenye simu ya mwenye gari, camera zenyewe kwenye hii picha zipo kwenye hiyo nguzo yenye miduara meusi pembeni mwa barabara.
 
UNAAMBIWA

Mtangazaji maarufu wa Marekani Steve Harvey hununua zawadi ya TV kila mwaka na kumpelekea Mwalimu wake wa zamani ambaye aliwahi kumwambia kamwe hatokuja kuonekana kwenye TV.

Steve anasema Mwalimu alimwambia kauli hiyo akiwa mdogo baada ya kuwapa Wanafunzi maswali ya kutaka waeleze wanataka kufanya kazi gani ukubwani au wanataka kuwa nani.

Steve ambaye alikuwa na tatizo la kigugumizi kikali wakati huo aliandika anataka kuwa Mtangazaji mkubwa atakayeonekana kwenye TV lakini Mwalimu akamwambia hiyo ni ndoto na haitowezekana.
 
UNAAMBIWA

Nchini Uingereza kuna shindano kila mwaka ambalo Washiriki kutoka Mataifa mbalimbali hupewa dakika 5 kila mmoja kusema uongo mkubwa ambao unaweza kuwashawishi Watu na wakahisi ni ukweli.

Wanasiasa na Wanasheria hawaruhusiwi kushiriki mashindano hayo kwasabababu inaaminika ni wazuri kwenye suala hilo la kushawishi uongo kuonekana ni kweli. ni uongo gani uliwai pigwa ukajua ni ukweli?
 
UNAAMBIWA

Kwenye rekodi za kesi zilizoripotiwa Polisi Nchini Uingereza imo pia ya Wezi wawili wa Laptop ambao walivunja nyumba na kuiba laptop na walipoifungua baadae walikasirishwa na video waliyoikuta ndani ya mwenye nyumba hiyo akifanya vitendo vya ngono na Mtoto, waliamua kuipeleka video hiyo Polisi na kukiri kuwa wao ni Wezi wa laptop.

Mwenye laptop alifungwa miaka mitatu jela kwa unyanyasaji we kingono na Jaji akawahukumu wezi kifungo cha nje na kufanya kazi za kijamii kwa miezi 12 na kusema hajawafunga jela kwakuwa walifichua makosa ya mwenye laptop.
 
Ndomana muda mwingine sio vizuri kuwakasirikia wanaotukatisha tamaa

Ni vile wanatu push kwenda na kufikia malengo yetu
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya watu wanaotoa maneno kuhusu chanjo ya maambukizi ya Uviko 19, akisema chanjo hiyo ni salama na ni tiba kwa wanaotumia.

Ameyasema hayo leo Septemba 7, 2021 wakati akihutubia katika mkutano wa wadau wa mifugo uliofanyika jijini Dar es Salaam, akieleza sababu ya Serikali huruhusu chanjo nchini.

“Chanjo hapa kwetu imekuwa na maneno maneno mengi.

Nataka niwaambie tupunguze maneno, hii ni tiba na tiba hii mtu hawezi kuithamini mpaka limkute kwenye familia ndiyo atajua umuhimu wa chanjo,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.


Waziri Mkuu amesema chanjo hiyo ni salama akisisitiza kuwa Serikali imeshajiridhisha.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…