Farhan Jr
Tayari Lionel Messi ameelekea PSG inayomilikiwa na Waarabu wa Qatar, chini ya Sheikh Tamim Bin Ahmad El Than ambaye pia ni Amir wa nchi ya Qatar
Muda wowote kuanzia sasa Cristiano Ronaldo atatambulishwa kama Mchezaji mpya wa Manchester City, inayomilikiwa na Tajiri wa Kiarabu Sheikh Mansour Bin Zayed El Naian wa Falme za Kiarabu
Maana yangu nini? Kuna siku Sir Alex Ferguson aliwahi kusema " One thing about football is not about football" akimaanisha kitu kimoja kuhusu mpira huwa hakihusu mpira
Kuna kitu kinaitwa ARAB SUPREMACY! Kule Mashariki ya kati kuna vita kubwa sana! Kila taifa la Kiarabu linataka utawala eneo hilo na Football ni sehemu moja wapo, wamehamishia ushindani hapo
Unaweza kuona ni suala la kimpira tu lakini ni zaidi ya mpira, on repeat! One thing about football is not about football