BIASHARA KUTUMIA UWANJA WA KIRUMBA
.
Klabu ya Biashara United imechagua kutumia Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kama uwanja wa nyumbani kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
.
Timu hiyo ambayo itashiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza imepangwa kuanzia hatua za awali ikianzia ugenini dhidi ya FC Dikhil ya Djibouti ambapo mchezo wa kwanza utapigwa kati ya Septemba 10 na 12, huku mechi ya marudiano ikichezwa Septemba 17-19, mwaka huu.
.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Seleman Mataso amesema kuwa tayari wameshawasilisha barua TFF, huku wakiwa wamepata baraka zote kutoka kwa wasimamizi wa Uwanja wa CCM Kirumba.