Makapuku Forum

PIQUE AIKOMBOA BARCELONA

Ikiwa tayari Barcelona ina 95% ya mishahara yote ilikuwa haiwezekani kuweka sajili zao mpya kama Memphis Depay na Eric Garcia

Ililazimika Mchezaji mmoja ajitolee kukatwa sehemu kubwa ya mshahara wake ili nyota hao waorodheshwe kwenye mfumo

Gerrard Pique alitoa ushirikiano mkubwa, amekubali kukatwa sehemu kubwa sana ya mshahara wake kufanikisha zoezi hilo

Licha ya watu wa kambi ya Pique walikataa sana ila yalikuwa maamuzi yake binafsi kwa mapenzi yake kwa Klabu yake

Hivi sasa Depay na Garcia tayari wameingizwa kwenye mfumo baada ya makato kwa Pique
 
KWANINI MABADILIKO YA NEMBO?

Nembo ni kitu muhimu sana katika utambulisho wa taasisi yoyote.

Inavutia watu kukufuatilia kwa umakini na kwa ukaribu zaidi.

Husaidia kutengeneza ushawishi wa haraka kwa mtu anayekiona kitu kwa mara kwanza yaani first impression.

Ni msingi mkuu wa utambulisho wa jina chapa yaani brand.

Hukutenganisha na washindani wako kibiashara.

Hutengeneza uaminifu kwa chapa yaani brand kwa wafuasi wake.

Kama klabu, sisi Azam FC tumezingatia yote hayo katika kufikia maamuzi ya kuja na nembo hii ambayo tumeizindua.

Wakati tukiwa katika mradi mpya kuelekea msimu mpya na misimu mingine mbele, ni matarajio yetu nembo hii itatusadia kutujengea taswira mpya na matumaini mapya.

Ahsanteni sana

-Mtendaji Mkuu wa Azam fc ndugu Abdulkarim aka Popat
 
Tammy Abraham atua Roma akiitosa Arsenal
.
Straika wa Chelsea Tammy Abraham amekubali kujiunga na AS Roma kwenye dili ambalo limeigharimu Roma Pauni milioni 34.
.
Hakuonekana kuwa kwenye mipango ya Thomas Tuchel kwa msimu huu na mkataba wake Chelsea ulitarajiwa kumalizika mwaka 2024.
.
Tammy ni miongoni mwa wachezaji wanaoonekana kukubalika sana na Jose Mourinho ambaye anaamini kutua kwenye kikosi atakuwa na msaada mkubwa kwenye eneo la ushambuliaji.
.
Mbali ya Roma, Abraham alikuwa akihusishwa kuwa huenda akajiunga na Arsenal lakini kutokana na kutokuwa na uwezo wa kutoa pesa hiyo wameshindwa kumsajili.
 
NSAJIGWA AULA STARS
.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemteua nahodha wa zamani waYanga naTaifa Stars, Shedrack Nsajigwa kuwa kocha msaidizi akisaidiana na Kocha Mkuu, Kim Poulsen katika kikosi kinachojiandaa na mechi za kuwania kufuzu ushiriki wa fainali za Kombe la Dunia 2022, huku Ivo Mapunda akibaki kuwa kocha wa makipa.
.
Nsajigwa anachukua nafasi ya Juma Mgunda na Seleman Matola waliokuwa makocha wasaidizi wa Stars huku Nadir Haroub‘Cannavaro’akiendelea kuwa meneja wa timu hiyo.
 
HAALAND NI MAN UTD TU
.
Habari ndo hiyo. Manchester United inatajwa kuwa klabu pekee kwenye Ligi Kuu England yenye nafasi kubwa ya kunasa huduma ya straika, Erling Haaland.
.
Man City na Chelsea zilihusishwa dirisha hili la uhamisho, lakini The Blues imemnasa Romelu Lukaku na Wananchi Man City wameelekeza nguvu kunasa saini ya Harry Kane, hivyo hawatasumbuka na saini ya Haaland, ambaye amesisitiza amekuwa mtu mwenye ndoto za kucheza Enland msimu ujao.
.
Kwa mujibu wa AS, Man United wamebaki wenyewe tu ambao wanaweza kunasa saini ya mkali huyo mwenye umri wa miaka 21. Watasubiri kukamilisha jambo hilo mwakani, wakati Haaland atakapokuwa akiuzwa kwa Pauni milioni 65 tu kutokana na kipengele kilichochowekwa kwenye mkataba wake.
.
 
BANDA kuibukia Ligi kuu Bara
.
Beki wa zamani wa Coastal Union na Simba, Abdi Banda aliyekuwa akikipiga Afrika Kusini katika klabu ya Highlands Park, yupo nchini kama mchezaji huru na sasa anapiga hesabu kuibuka kwenye Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao unaoanza Septemba 27.
.
Banda amesema kuwa yupo nchini kwa sasa na anataka aitumikie timu yoyote ya Ligi Kuu Bara kwa msimu mmoja, kisha aangalie ustaarabu mwingine na hakutaka kuweka wazi ni wapi anakwenda.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…