Makapuku Forum

Makapuku Forum

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Albert Chalamila amekabidhi rasmi Ofisi leo kwa Mkuu wa Mkoa mpya wa Mwanza Robert Gabriel.

Uteuzi wa Chalamila umetenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mabadiliko madogo ya Wakuu wa Mikoa aliyoyafanya ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amehamia Mkoa wa Mwanza kuchukua nafasi ya Chalamila huku RC wa Tabora Ally Hapi akienda Mara kuwa RC akichukua nafasi ya Gabriel.
20210611_135238.jpg
20210611_135258.jpg
20210611_135316.jpg
 
Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere amemtembelea Mjane wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Tano, Dr. John Pombe Magufuli, Mama Janeth Magufuli nyumbani kwake Dar es salaam leo.
20210611_135535.jpg
 
Mtangazaji Fred Fidelis maarufu kama Fredwaa amefariki dunia leo Dar es salaam, taarifa za awali zinasema amefariki baada ya kupata ajali leo Kawe, Dar es salaam… taarifa zaidi kukujia.

Fredwaa amewahi kufanya kazi Times FM Dar es salaam, Radio Free Africa Mwanza pamoja na CloudsFM Dar es salaam
20210612_192416.jpg
 
Serikali ya Marekani kupitia Ubalozi wake wa Tanzania imetangaza kwamba itanunua dozi milioni 500 za chanjo ya COVID-19 aina ya Pfizer COVID-19 na kuzitoa msaada kwa Nchi mia moja (100) zenye kipato cha chini duniani.

Taarifa hiyo ya Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania imesema "Hii ni ahadi na msaada mkubwa unaotolewa na Watu wa Marekani kuwasaidia Watu duniani kote"

Mpaka sasa covid-19 imesababisha vifo vya Watu milioni 3.78 huku Wagonjwa wakifikia milioni mia moja sabini na tano.
20210612_193205.jpg
20210612_193229.jpg
 
"Dar es salaam kwa sasa wako salama wanafanya kazi vizuri, uhalifu utaendelea kuwa historia, nikushukuru Rais Samia kwa kunipa heshima na kunikumbuka kunipa Ukuu wa Mkoa wa Dar es salaam”———Amos Makalla

“Rais Samia nakuahidi sitokuangusha, nimeanza sio kwa kutembea ni kwa kukimbia kwasababu umenirudisha nyumbani Mimi ni Mtoto wa hapahapa Dar es salaaam, nimezaliwa hapa nimekulia hapa na kama shughuli imempata Mwenyeji, nitakusaidia kuona matarajio na imani uliyonayo kwangu vinatimia”———Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla
20210612_193332.jpg
 
Mwanamume mmoja anayefahamika kwa jina la Nehemia Muhamed (40) Mkazi wa Kijiji cha Nyankoronko Wilayani Buhihgwe Mkoani Kigoma anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua Mke wake kwa kumkatakata na panga na kutengashia mwili wake.

Kamanda wa Polisi Kigoma ACP James Manyama amesema Mwanamke aliyeuwawa anaitwa Adela Ndihagati (40 ) ambaye aliuwawa nyumbani kwake huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

“Kwa sasa anauguza majeraha aliyopata akitaka kujidhuru, kwenye Hospitali ya Buhigwe chini ya ulinzi mkali na upelelezi utakapo kamilika Mtuhumiwa anafikishwa Mahakamani kujibu shitaka lake” ——— RPC Manyama.
20210612_194009.jpg
 
Mtangazaji Fred Fidelis maarufu kama Fredwaa amefariki dunia leo Dar es salaam, taarifa za awali zinasema amefariki baada ya kupata ajali leo Kawe, Dar es salaam… taarifa zaidi kukujia.

Fredwaa amewahi kufanya kazi Times FM Dar es salaam, Radio Free Africa Mwanza pamoja na CloudsFM Dar es salaam View attachment 1816380
Pole yao sana wafiwa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom