Hizi ni picha za Mkuu wa zamani wa Majeshi wa Uganda Jenerali Katumba akiwa na Mtoto wake aitwae Brenda kabla ya kifo chake leo, Brenda amefariki leo baada ya Watu wasiojulikana kulishambulia kwa risasi gari walilokuwemo ambapo pia Dereva naye amefariki, Jenerali Katumba amejeruhiwa na amelazwa Hospitali.
“Brenda amerudi hivi karibuni kutoka Marekani ambako amehitimu masomo yake, inaumiza sana sijui Serikali itafanya nini kuhusu tukio hili maana Katumba hajafanya lolote baya kustahili mateso haya”———Joyce Sentongo, Ndugu wa Katumba.
Jenerali Katumba Wamala ambaye amekuwa Waziri wa uchukuzi na ujenzi kwenye Serikali ya Rais Yoweri Museveni ya muhula wa tano anatambulika kama Mtu asiyependa makuu na hatembei na msafara wa Walinzi kama wenzake walio kwenye ngazi za juu za Serikali.
Rais Samia amerejea Dodoma leo akitokea Dar es Salaam, amepokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka ambapo kesho June 02, 2021 Rais Samia atawaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Ikulu Chamwino kuanzia saa 4:00 asubuhi.