Norway ni miongoni mwa Nchi chache ambazo Magereza yake hayafanani na Magereza mengine duniani, Nchi hii inaamini kwenye kutoa mafunzo zaidi badala ya adhabu pale Mtu anapofungwa, hili ni moja ya Magereza yao likiwa na Library, Gym na jiko zuri kwa ajili ya Wafungwa.
Utafiti wa Emory University na National University of Singapore unaonesha moja ya sababu kubwa zinazovunja Ndoa nyingi za kifahari ni mifarakano inayotokana na madeni ya sherehe zenyewe ambapo Wanandoa hujikuta wenye stress za madeni na kuanza kulaumiana.
Wataalamu pia walishauri Wanandoa wasifanye sherehe za gharama sana bali za kiwango cha kawaida kuanzia kwenye pete za uchumba ambazo walishauri zianzie $500-$1000 (Tsh. milioni 1.1-milioni 2.3).
Huko Fukuoka Japan kuna Hotel ambayo Mteja analipia $ 1 tu kwa siku (Tsh. 2,318) lakini kwa sharti moja la kukubali kuoneshwa Live kwenye YouTube ya Hotel akiwa chumbani na maeneo mengine ya Hotel, hii huwezesha Watu wa Hotel kupata pesa kupitia matangazo ya Youtube.
Tetsuta Inoue aliwaza ni kitu gani cha ubunifu atafanya kuendesha Hotel kuliteka soko la digitali ambapo Mteja akiwa chumbani Live huruka bila sauti ili aongee na simu na maongezi mengine, anaruhusiwa kuzima taa akiwa anavaa au akiwa na Mpenzi, bafuni hakuna camera.