Makapuku Forum

Makapuku Forum

Simba nguvu moja
20210508_140208.jpg
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba SC na Yanga SC iliyokuwa ianze saa 11 jioni sasa itaanza saa 1 usiku.

TFF imesema imepokea maelekezo ya mabadiliko ya muda wa kuanza mchezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Tayari timu husika zimeshapewa taarifa ya mabadiliko hayo kupitia Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).
20210508_170938.jpg
 
Wachezaji wa Yanga SC wamewasili Uwanja wa Benjamini Mkapa, wametumia geti lisilo rasmi Uwanja wa Uhuru na kupitia Media Centre, Yanga wamesisitiza kuwa mechi wanayoitambua wao ni saa 11 jioni na sio saa 1:00 usiku.
20210508_171441.jpg
 
Yanga wameshapanga cones na mipira tayari ipo uwanjani kwa ajili ya warm up licha ya mchezo kusogezwa hadi saa 1:00 usiku.
20210508_171619.jpg
 
Wananchi tayari wamefanya warm up, mpango wao bado ni kucheza mechi saa 11:00. Wakati wao wakifanya warm up, Simba bado haijawasili uwanja wa Mkapa.
20210508_171716.jpg
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesitisha utekelezaji wa kanuni ya kuhakiki nyimbo za Wasanii kabla ya kupelekwa kwenye Vyombo vya Habari na kwa Walaji wengine, ametoa uamuzi huo leo Dar es salaam alipokutana na Wasanii pamoja na Wadau wengine wa Sanaa.

Uhakiki huu ulianza hivi karibuni baada ya utekelezaji wa kanuni ya kuzipitia nyimbo na filamu mpya kabla ya kurushwa, kuanza kutumika kuanzia May 01,2021 lakini baadaye ulilalamikiwa na Wasanii na Wadau wengine wa sanaa kwamba unawakwamisha Wasanii.
20210508_172111.jpg
 
Wananchi wa Vijiji vya Nyiboko, Borenga, Machanchari na Maremboto vilivyopo Kata ya Kisaka wilayani Serengeti wameliomba Jeshi la Wananchi (JWTZ) kukagua na kuondoa mabomu yaliosalia maeneo ya makazi baada ya Watoto kuokota bomu ambalo halijalipuka mara baada ya kuhitimisha mafunzo ya kivita.

Akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha Wananchi, Viongozi wa Serikali ya Vijiji vinne, Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa JWTZ , Mzazi mmoja amesema Jeshi limekuwa likitumia eneo hilo kufanyia mazoezi, ambapo aliwaona Watoto wake wameshika bomu wakichezea na yeye akalichukua na kulitupa porini.

Mkuu wa Kikosi cha Makoko Kanali Samson Mshasha amesema ni kweli bomu hilo lilisahaulika ila amewaomba Wananchi wahame ili kujiweka salama, kwani 1996 Wananchi walikubali kutoa eneo kwa matumizi ya Jeshi ila kwa sasa wameanza kujenga nyumba (kutegesha) ili walipwe fidia kinyume na taratibu kwani kuna vifaa na silaha huwa zinabaki kwa bahati mbaya wakati wa mazoezi, pia amewataka Wananchi kutoa taarifa waonapo silaha na vifaa vingine vya kijeshi.

DC wa Serengeti Nurdin Babu, amesema kila Mwananchi aheshimu mipaka ya eneo la Jeshi na kuwataka waliokutwa na Jeshi wajitokeze watambulike ili utaratibu wa kuwalipa ufanyike ila waliotegesha nyumba ili walipwe hawatalipwa kwani ramani ipo na inaonesha vizuri.
20210508_172331.jpg
20210508_172353.jpg
 
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) leo Alfajiri limezindua rasmi safari za moja kwa moja Kutoka Dar es salaam hadi Guangzhou, China baada ya kuahirishwa mara kadhaa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo janga la Corona.

Uzinduzi huo umeongozwa na Mhandisi. Dkt. Leonard Madaraka Chamuriho, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi.

Hizi ni picha kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 3, Raia wa China wakiwa kwenye maandalizi tayari kuanza safari.
20210508_172704.jpg
20210508_172731.jpg
20210508_172751.jpg
 
“Nakushukuru sana Mzee wangu Rais Mstaafu Mwinyi kwa kunikaribisha kuzindua kitabu cha simulizi ya maisha yako, nampongeza Mzee Mwinyi kwa kuamua kuandika kitabu ambacho sio tu kitawasaidia Watanzania na Dunia kumfahamu pia kina historia ya Tanzania”———Rais Samia kwenye uzinduzi kwa kitabu cha Mzee Mwinyi Dar es salaam leo

“Hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Mzee Mwinyi inaenda sambamba na kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa, tunamtakia kila la kheri wakati anatimiza miaka 96, tunamuomba Mungu akutunze ufike miaka 100 na zaidi ili tuzidi kuvuna hekima na busara zako”———Rais Samia

“Nimemuandalia zawadi Mzee Mwinyi, kwa kutimiza umri wa miaka 96 leo, nimekuwa nikiona usumbufu anaoupata akiwa anapanda na kushuka kwenye Gari lake, kwa niaba ya Serikali Mzee wetu leo tutampatia Benz la chini ambalo litampa raha kwenye Safari zake”———Rais Samia
20210508_182926.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom