Leo tunarudi Tanzania nimekutana na haya maajabu ya ziwa lenye rangi nyekundu kama damu.
Ziwa hili linaitwa ziwa Natron, lenye joto linalofikiwa kuwa digrii 60 za sentigredi na uwepo wa chumvi kali ya kufa mtu, linavutia sana na hata wakati mwingine unaweza kujisikia kutaka kuogelea ndani yake hasahasa kipindi ambacho unasikia joto, lakini mahali hapo si pa mzaha hata kidogo.
Rangi ya ziwa hili imekuwa kivutio si tu kwa binadamu ila hata kwa wanyama mbalimbali, ila cha kustaajabisha na kuogopesha ni kuwa wanapothubutu kutia mdomo au kuingia kwenye maji hayo hapo hapo wanageuka kwa kukauka na kuwa kama jiwe.
Lakini licha ya hivyo kuna baadhi ya viumbe ambao hawadhuliki katika ziwa hilo, ndege aina ya flamingo na pia kuna baadhi ya samaki hawadhuliki na kiasi kikubwa cha alkaline ipatikanayo katika hili ziwa ndio kwanza wanazaliana kwa wingi.
Watu wengi wanajiuliza ni kitu gani hupelekea viumbe vinavyothubutu kusogelea hili ziwa kukakamaa au kuwa kama majiwe. Watafiti wanaeleza kuwa hili ziwa linakiasi kikubwa cha alkaline na kaustic soda/ magadi ambacho huingia ndani ya mwili wa hicho kiumbe na kupelekea kufa na kukakamaa kabisa.