Makapuku Forum

Mkutano unaohusu masuala ya Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) umefanyika Maputo, Msumbiji chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Msumbiji Fellipe Nyusi.

Marais kutoka Nchi tano ikiwemo Afrika Kusini, Botswana, Malawi na Mwenyeji Msumbiji wamehudhuria ambapo kwa upande wa Tanzania Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi amemuwakilisha Rais Samia Suluhu katika mkutano huo.

Nyusi amezishukuru Nchi Wanachama na kuwaomba kuendelea kuzidisha ushirikiano katika kuhakikisha hali ya usalama inaimarishwa zaidi sio tu katika eneo la Cabo Delgado lililokumbwa na tishio la ugaidi bali kwenye Jumuiya yote.

Mapema Mtendaji wa SADC Dkt. Stargomena Tax alisema suala la ugaidi ni gumu na haliwezi likaachiliwa kwa Nchi moja pekee.
 
Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza jana hatua sita za Rais ambazo Serikali yake itazichukua katika juhudi za kukabiliana na kile alichokiita janga la mashambulizi ya silaha ambalo limeshika kasi Marekani.

Biden ameyaita mashambulizi ya silaha kuwa ni mzozo wa kiafya wa kitaifa unaoigharimu Marekani, sio tu kimaisha na mustakabali wa Raia wake, lakini pia unaigharimu Marekani kiasi kinachokadiriwa kufikia Dola Bilioni 280 kila mwaka.

Akizungumza nje ya Ikulu ya White House, Biden amesema ni lazima mashambulizi ya silaha ambayo yanaripotiwa kila kukicha yafikie mwisho.

Miongoni mwa hatua ambazo atazisaini mara moja ni pamoja na kuwataka Watu wanaonunua vifaa na kuunda silaha nyumbani kuchunguzwa kwanza historia zao, ama wale wanaotaka kuzifanya silaha zao kuwa kali zaidi kuwasilisha majina kwenye mamlaka kabla ya kuruhusiwa kununua vifaa hivyo.
 
Rais Uhuru Kenyatta amezindua kiwanda cha utengenezaji bunduki ambacho ni sehemu ya viwanda vya vifaa vya usalama wa kitaifa eneo la Ruiru Kaunti ya Kiambu, Kenya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kenyatta amesema kiwanda hicho kitasaidia katika kuimarisha uchumi wa kitaifa na ufanisi wa kiteknolojia Kenya.

Amesema kiwanda hicho pia kitapunguza gharama ya ununuzi wa silaha nje ya Nchi (kwa hadi 60%) na kuwezesha sekta ya usalama kuwa huru huku akisema Kenya itaendelea kuimairisha utengenezaji wa vifaa vya kisasa vya usalama.
 
Prince Philip ambaye ni Mume wa Malkia Elizabeth II, amefariki duniani akiwa na umri wa miaka 99, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amethibitisha taarifa hizo na kuelezea masikitiko yake kufuatia kifo hicho.
 
Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika, SADC, wamesema watakabiliana na Wapiganaji wa siasa kali walioushambulia Mji muhimu wa Kaskazini mwa Msumbiji mwezi uliopita, kwa kutumia nguvu sawasawa na kitisho cha Kundi hilo.

Uamuzi huo umetokana na Mkutano wa Viongozi wa Nchi sita za Zimbabwe, Afrika Kusini, Malawi, Msumbiji, Botswana na Tanzania waliofanya kikao cha dharura Maputo,Msumbiji jana, wiki mbili baada ya shambulio hilo katika mji wa Palma, ambalo liliuwa makumi ya Watu na kulazimisha maelfu ya wengine kuyakimbia makaazi yao, Rais wa Zanzibar Dr.Mwinyi na Waziri Mulamula walimwakilisha Rais Samia kwenye Mkutano huo.

Tangazo lililochapishwa baada ya Mkutano huo, lilisema shambulizi hili lililotajwa kuwa la kihalifu haliwezi kuachwa bila kujibiwa na ukanda wa SADC.

Tangazo hilo limeongeza kuwa Timu ya Watalamu itapelekwa haraka Maputo, ingawa haikuelezea muundo wa Timu hiyo wala majukumu yake.
 
Staa wa zamani wa Simba SC Emmanuel Okwi leo ameungana na kula chakula cha pamoja na wachezaji wenzake wa zamani wa Simba SC Jijini Cairo wanaosubiria kuivaa Al Ahly leo 22:00 EAT, Okwi anaichezea Ittihad Alexandria ya mjini Alexandria ambapo ni umbali wa saa 2 na nusu hadi Cairo
 
Korti Kuu ya Kenya imesimamisha hatua ya serikali ya nchi hiyo ya kuzifunga kambi mbili za wakimbizi ambazo zinahifadhi mamia kwa maelfu ya wakimbizi kutoka nchi jirani zinazozongwa na mizozo ya kivita.

Jaji Antony Mrima wa mahakama hiyo ametoa amri ya kuisitisha hatua hiyo ya serikali kwa muda wa siku thelathini, kufuatia ombi la mmoja wa wanasiasa wenye ndoto za kuwania urais wa Kenya, Peter Gichira.

Awali, waziri wa mambo ya ndani wa Kenya, Fred Matiang'i, alikuwa amelipa shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wakimbizi, UNHCR, muda wa siku 14 wa kuzifunga kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma, akisema hakuna uwezekano wowote wa kujadiliana kuhusu uamuzi huo.

Muda huo ulimalizika jana. Kambi ya Dadaab inao wakimbizi wapatao 200,000 wengi wao wakiwa kutoka Somalia, nayo ya Kakuma inahifadhi takiribani idadi kama hiyo, wengi wao wakiwa ni wakimbizi wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini.
 
Upo Shunie?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…