“Naipongeza Kampuni ya Kichina kwa kushinda zabuni ya ujenzi wa reli ya kisasa Kilometres 341 kutoka Mwanza hadi Isaka( mradi una gharama ya Tril 3.0677), nina matumaini watafanya kazi kubwa”-JPM mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi leo Chato
“Nimemuomba Waziri Wang Yi, akafikishe salamu zangu kwa Rais Xi Jinping kwamba watusamehe madeni yakiwemo ya USD Mil. 15.7 ya deni tulilobeba wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA, deni la USD Mil.137 la nyumba za askari pamoja na deni la kiwanda cha Urafiki la USD Mil.15, nimeomba watufutie kwasababu China ni Rafiki zetu, pia wao ni Matajiri”-JPM
“Nimewaeleza hali halisi kwamba China ni Nchi Tajiri Duniani, na sisi Tanzania tuna mazao mengi, ndio maana kwenye zawadi zangu nimetoa korosho, chai na kahawa, nataka wakaanze kula korosho za Tanzania badala ya Nchi nyingine, huu ndio wakati wa kulishika soko la China”-JPM
“Nampongeza sana Waziri Wang Yi kwasababu hajavaa barakoa maana anajua Tanzania hakuna Corona na kwa kumuhakikishia nakwenda kumshika mkono tukale chakula