Tumosa
JF-Expert Member
- Jul 21, 2016
- 16,527
- 52,623
TUOMBE:Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu BWANA MUNGU WA MAJESHI..ASANTE BABA KUTUAMSHA SALAMA LEO Alhamisi njema tarehe 28 Februari 2019 ..Asante kwa neema na rehema...Tunaomba toba kwa makosa yote tuliyofanya kwa mawazo ,maneno,matendo na kwa kutotimiza wajibu mbalimbali...uturehemu twakusihi.Siku ya leo tunaleta kila hitaji mbele yako maana hatuna mahali popote tunapopategemea..tunaomba utuponye magonjwa yetu yote
tusaidie tukuone Baba katika kila tutakachofanya leo fungua milango ya baraka kwa kila mmoja wetu.Tunaomba uponyaji wa mwili na roho.Bariki kuingia na kutoka kwetu..tupe imani thabiti katika kila jambo tukushirikishe.... kila mapito yetu. Tukuite Mfalme was Amani ..adui mwovu ashindwe katika jina la Yesu Kristo...Wabariki wasafiri...waangalie na kuwafariji wafiwa wote wape tumaini.angalia wajane,yatima na wote wanaohitaji msaada kimwili na kiroho wakuangalie wewe tu.
Tusaidie tuwe msaada kwa kila mmoja ,tuongeze upendo na imarisha amani katika maeneo yote na kwa kila jambo tukutangulize.Asante Baba kwa kuwa utatenda sawa na mapenzi yako.Tunaomba yote katika jina la Yesu Kristo Mpatanishi na Mwokozi wetu Amen.
ALHAMISI NJEMA YA UPENDO DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE







